Shinyanga: Mzee wa miaka 70 ashambuliwa na fisi akiwa amelala usiku

Shinyanga: Mzee wa miaka 70 ashambuliwa na fisi akiwa amelala usiku

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkazi wa Kijiji cha Chela katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga, Buluba Jilasa (70) amejeruhiwa na fisi kwa kung’atwa sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa amelala.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Halamashauri ya Mji wa Kahama Jilasa amesema tukio hilo limetokea jana usiku wakati akiwa amelala, nyumbani kwake alishituka mlango ukivunjwa na fisi huyo ambaye aliingia hadi chumbani na kuanza kumjeruhi.

“Nimepambana naye ili asimdhuru, lakini alifanikiwa kuning’ata kiganja cha mkono wa kushoto na kunisababishia majeraha makubwa katika maeneo mbalimbali ya mwili wangu” alisema Jilasa.

Amesema aliweza kumdhibiti fisi huyo ambaye baadae alianza kushambulia kuku na ndipo alipotoka na kwenda kumgongea mjukuu wake Charles Bushemeli kwa ajili ya kuomba msaada.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chela Zaphline Samweli amesema tukio la fisi kuvamia kwenye mkazi ya wananchi sio la kwanza na wamekuwa wakivamia nyakati za usiku na kushambulia mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi pamoja na punda kutokana na uwepo wa milima mingi.

Amesema mapango yaliyopo kwenye milima iliyopo kijijini hapo ndio makazi ya wanyama hao wanapojificha na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari na kutoa taarifa kwa maafisa maliasili pindi wanapowaona wanayama hao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama Dk George Masasi amethibitisha kumpokea majeruhi huyo ambaye alikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na ameshaapatiwa huduma ya matibabu na anaendelea vizuri.

“Tumemchoma sindano ya kuzuia asipate kichaa kinachotakana na kung’atwa na fisi(Anti Rabies)na mkono wake wa kushoto umeshambuliwa vibaya unatakiwa kukatwa kiganja" alisema Masasi.

1574338165265.png
 
Matukio ya fisi kuua watu mara zote yanatokea kwa wingi Kanda ya Ziwa! Hivi hao fisi huwa wanafugwa huko, au wanatokea hifadhini.

Watu wa Kanda ya Ziwa tafadhali, naombeni mnisaidie kwenye ufafanuzi.
 
Matukio ya fisi kuua watu mara zote yanatokea kwa wingi Kanda ya Ziwa! Hivi hao fisi huwa wanafugwa huko, au wanatokea hifadhini.

Watu wa Kanda ya Ziwa tafadhali, naombeni mnisaidie kwenye ufafanuzi.
Kule fisi kitu cha kawaida sana. Usiku wanalia balaa unawasikia, sijui kwanini.
 
Fisi ni Kati ya wanyama waoga sanaa..na ninashangazwa kusikia fisi kumshambulia binadamu ingali fisi porini ata kuwinda mnyama swala huwezi yeye vyake mizoga tuu. Hao watakuwa fisi wa kutengenezwa kwakweli so kawaida
 
Usiombe ukutane na Fisi mwenye njaa mkuu. Njaa mbaya sana mkuu,wewe siunaona hata binadamu akizidiwa anavyochanganyikiwa na kuanza kuhama hama.
 
Matukio ya fisi kuua watu mara zote yanatokea kwa wingi Kanda ya Ziwa! Hivi hao fisi huwa wanafugwa huko, au wanatokea hifadhini.

Watu wa Kanda ya Ziwa tafadhali, naombeni mnisaidie kwenye ufafanuzi.
Hao ni fisi wa kishirikina maana fisi halisi wa porini ni mwoga sio rahisi kuvamia hivyo ! Angekua wa kawaida wanakijiji wangevamia hayo mapori na kuwasaka fisi wote
 
Mkuu kikoa ya Shinyanga na Simiyu, fisi ni wengi kama panya.

Mchana wanajificha mapangoni na kwenye mashimo.

Ikifika sa12 jioni, hutokeza na kuanza kutafuta mawindo.
..lakini mkuu hizo nyumba za wenzetu zikoje yani fisi anakuja usiku anavunja mlango anaingia ndani na kuvunja mwingine wa kuingia chumbani na kuanza kushambulia watu!!
 
..lakini mkuu hizo nyumba za wenzetu zikoje yani fisi anakuja usiku anavunja mlango anaingia ndani na kuvunja mwingine wa kuingia chumbani na kuanza kushambulia watu!!
ukipewa jibu
Naomba uni tag mkuu
 
Fisi ni Kati ya wanyama waoga sanaa..na ninashangazwa kusikia fisi kumshambulia binadamu ingali fisi porini ata kuwinda mnyama swala huwezi yeye vyake mizoga tuu. Hao watakuwa fisi wa kutengenezwa kwakweli so kawaida
Fisi huwajui vizuri mzee. Hiki ulicho andika ni story tu.

Fisi anapola nyama chui, Duma etc.

Fisi ingawa n mdogo kwa Simba bt huwa Simba akiingia vibaya fisi wanna mtiririsha.

Fisi akiwa na njaa, hashindwi kuingia ktk kundi la Simba angalau apate nyama wanayo Kula. Fisi kichaa mno, yeye akikuta mnyam huwa hauui, ana mla hivyo hivyo akiwa mzima.

Chukua elimu mpya hii
 
Hicho kijiji cha chela kimezungukwa na milima (siga Hills ) maeneo hayo yana fisi wengi kutokana na milima hiyo inayoitwa kwa kisukuma " lyandi lya Baloha " na kwa sasa haina wanyama wengi wa porini, hivyo lazima fisi wavamie watu.
 
Back
Top Bottom