Shinyanga: TMDA yakamata shehena ya sigara bandia kutoka Kongo, yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 1

Shinyanga: TMDA yakamata shehena ya sigara bandia kutoka Kongo, yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 1

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba Tanzania (TMDA) kanda ya ziwa magharibi, imekamata shehena ya sigara bandia aina ya SuperMatch yenye thamani ya Sh1.8 bilioni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 28, 2022 na Meneja wa kitengo cha Uhusiano TMDA, Gaudensia Simwanza imeeleza walipokea taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Shinyanga.

“TMDA kanda ya ziwa magharibi baada ya kupokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku lililozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga, imebaini sigara hizo ni bandia na zimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Kongo ambapo kuna makasha 2200 yenye thamani ya Sh1.8 bilioni.

“Makasha hayo yana uzito wa tani 13.2 kazi hii tulishirikiana kwa karibu sana na MCIE, lakini cha kujiuliza zimepitaje mipakani na tunao wakaguzi huko? Hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na mzigo huu umezuiliwa,” amesema Simwanza.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna kipindi miaka ya 2000 nilipata mchongo wa sigara Benson & hedges toka Malawi kupeleka Mombasa nilipiga sana hela nilipewa mchongo na jamaa alikuwa tanga mjini ni marehemu kwa sasa hizo sigara zilikuwa feki l
Sasa ebu fafanua, feki kivipi, hazina tumbaku Kuna nyasi? Sielewi zinakuwaje feki.
 
Back
Top Bottom