Wakazi wa Kijiji cha Bushimani kata ya Chambo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Boma la Zahanati walilolijenga kwa nguvu zao mwaka 2012 ili kuwaondolea adha ya kufuata huduma za Matibabu umbali wa kilomita 10.
Veronica Michael na Elizabeth Mabula ni baadhi ya Wakazi wa Kijiji hiki wamepaza sauti kwa serikali ili kuwasaidia kuondokana na kero hiyo baada ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani kutembelea Boma la Zahanati hiyo na kutamka Neno la Faraja.