Shinyanga: Watoto waliotumwa dukani usiku, wabakwa, walawitiwa, waliwa na fisi (ripoti ya Polisi)

Shinyanga: Watoto waliotumwa dukani usiku, wabakwa, walawitiwa, waliwa na fisi (ripoti ya Polisi)

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Watoto 10 wakazi wa Kata ya Mhongolo, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, wamebakwa na kulawitiwa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita na wengine wawili wakiliwa na fisi.

Waliofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka sita hadi 12 wa jinsia ya kike na walikutwa na mkasa huo baada ya kuagizwa na wazazi wao dukani nyakati za usiku.

Watoto wawili wa kike walioliwa na fisi wanatoka katika Kata za Ngogwa na Wendele huku sababu ikitajwa kuwa ni kutokana na kuwapo mashamba makubwa ambayo wanyama hao wanajificha.

Mkaguzi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Tiho Masatu, aliyabainisha hayo jana Machi 28, 2022 wakati akitoa taarifa ya matukio ya vitendo vya Ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi, mwaka huu.

Alisema wazazi na walezi wamekuwa wakichangia kusababisha watoto wao wa kike kufanyiwa vitendo vya kikatili hususani kubakwa na kulawitiwa na watu wasiojulikana kwa kuwaagiza nyakati za usiku kwenda dukani kufuata mahitaji ya nyumbani.

"Vitendo vya ubakaji na ulawiti vimekithiri sana katika Kata ya Mhongolo eneo la Mtaa wa Mbulu na sababu kubwa inaonyesha ni vitendo vya wazazi kuwa na tabia ya kuwatuma watoto madukani hususani nyakati za usiku,” alisema Masatu.

Aliwataka wazazi kuhakikisha wanakuwa makini katika kulinda watoto wao hususani wa jinsia ya kike ili kuepukana na vitendo hivyo.

Kuhusu watoto kuliwa na fisi, Masatu alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori wameanzisha msako wa kuwatafuta wanyama hao ili kuwatokomeza.

Hata hivyo, alisema mpaka sasa hakuna hata mnyama mmoja aliyekamatwa na kuuliwa na kwamba wamekuwa wakifanya kazi hiyo mara kwa mara.

Masatu aliitaka jamii kuacha kuhusisha matuki hayo na imani za kishirikiana na kuwataka kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanawatokomeza wanyama hao.

Chanzo: Nipashe
 
Watoto 10 wakazi wa Kata ya Mhongolo, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, wamebakwa na kulawitiwa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita na wengine wawili wakiliwa na fisi...
Chanzo kikubwa ni kukosekana umakini kati ya wazazi. Yaan mijitu inazaazaa tu ili mradi imezaa. Haijali watoto kabisa

Mhongolo ni maporini kabisa sasa unamtumaje mtoto wa miaka chini ya 12 dukani usiku. Na maduka yako mbali mbali, huduma za umeme bado hazijafika mahala pengi sehemu hizo. Tangu miaka ya 2008 kuna kesi za kuwepo na fisi maeneo hayo coz kumejaa makolongo na sauti za fisi huwa zinasikika kabisa mida ya usiku.

Kuliko kuleta viumbe kwenye mateso bora usizae tu.
 
Usukumani kwa mafisi hawajambo! Sijui wanatafuta yanawasaidia nini
 
Back
Top Bottom