BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Walioshtakiwa ni Abel J. Kitinya (Mlinzi wa Mahakama ya Mwanzo Shinyanga), Janeth W. Lugano (Mwinjilisti), Mariam W. Kiloba (Mfanyabiashara) na Magreth W. Kiloba (Mfanyabiashara).
Mshtakiwa Abel Joseph Kitinya amesomewa Mashtaka ya kujihusisha na vitendo vya Rushwa na Kughushi Nyaraka. Washtakiwa 2, 3 na 4 wanakabiliwa na Makosa ya kuwasilisha Nyaraka za Uongo na kujipatia Tsh. Milioni 22,166,666 kila mmoja.
Kesi hiyo yenye Usajili wa CC. No. 6/2023, chini ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeahirishwa hadi Machi 28, 2023 itakaporejea Mahakamani kwa ajili ya kusoma hoja za Awali.