Shinyanga: Watumishi sita wafukuzwa kazi kwa utoro, kughushi

Shinyanga: Watumishi sita wafukuzwa kazi kwa utoro, kughushi

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi watumishi sita kutokana na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23, 2022.

Mboje amesema Baraza la Madiwani limewafukuza watumishi hao baada ya kupitia utetezi wao na baadhi yao hawajaonekana kutokana na kutokuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

“Baraza la Madiwani limewafukuza kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoka Idara ya Afya watumishi wawili wamefukuzwa kazi na kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni wanne,” amesema Mboje.

Mbali na watumishi hao sita kufukuzwa kazi, pia watumishi wengine wawili Baraza hilo limeagiza wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao na watafanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu.

Watumishi Idara ya Afya waliofukuzwa kazi ni Daktari Fidelis Benedict Mushi wa Kituo cha afya Nindo na Andrew Israel Mwakisambwe ambaye ni Mteknolojia Maabara Kituo cha Afya Salawe.

Watumishi wanne kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni Maafisa Watendaji wa Vijiji ambao Charles Dominick Mayunga (Bukene), Mercy Gasper Kyando (Kilimawe), Omary Hamis Omary (Igembya) na Robert Surika Mbuti (Mwabagehu).

SABABU ZA KUFUKUZWA…
Akitolea ufafanuzi zaidi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje alisema:

“Sababu za kufukuzwa zinatofautiana, wapo ambao wamefukuzwa kwa utoro kazini, wengine kwa kughushi nyaraka za kupata fedha.

“Wale wa utoro wengine walitafutwa hawakupatikana, hata walipotumiwa barua hawakujibu, hivyo wakawa wanatengeneza kosa juu ya kosa.

“Ambao wamekatwa mishahara ni kwa kuwa walighushi nyaraka ambazo ni barua na sahihi kwa ajili ya kuchukua fedha ambazo kweli zilienda kufanyia kazi ambazo zimeonekana, kamati iliyokuwa ikichunguza suala hilo imeona, lakini kwa kuwa walifanya makosa maana yake mishahara yao itakatwa hukohuko hazina na siyo sisi tutakaokata.”
 
Makosa gani wamefanya na utetezi wao ni upi?

Hiyo sheria ya kukatwa 15% ya mshahara wao ni sherua gani na hiyo hela inaenda kufanya nini maana kwa miaka 3 ni sawa na mkopo mkubwa tuu kwa mwenye mshahara wa 840,000 ni sawa na 4,530,000.

Pia haina usawa maana wanaweza kua na mshahara tofauti.
 
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi watumishi sita kutokana na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23, 2022.

Walio na Moshi wa zama za mwendazake wangalipo.

Daktari, jamaa wa maabara na hawa warugaruga wapi na wapi?
 
Makosa gani wamefanya na utetezi wao ni upi?

Hiyo sheria ya kukatwa 15% ya mshahara wao ni sherua gani na hiyo hela inaenda kufanya nini maana kwa miaka 3 ni sawa na mkopo mkubwa tuu kwa mwenye mshahara wa 840,000 ni sawa na 4,530,000.

Pia haina usawa maana wanaweza kua na mshahara tofauti.
Marekebisho ya mwaka 2019, so kuwa mpole mkuu tii sheria.
 
Soon wataanza kulia lia wana upungufu wa watumishi wakati wangeweza kudili nao kwa namna nyingine. Na maisha yakaendelea
 
Makosa gani wamefanya na utetezi wao ni upi?

Hiyo sheria ya kukatwa 15% ya mshahara wao ni sherua gani na hiyo hela inaenda kufanya nini maana kwa miaka 3 ni sawa na mkopo mkubwa tuu kwa mwenye mshahara wa 840,000 ni sawa na 4,530,000.

Pia haina usawa maana wanaweza kua na mshahara tofauti.
Sheria ya Utumishi wa Umma sura ya 298 marejeo ya Mwaka 2019.
 
Dah.......Wana makosa gani hao jamaa!??
ina maana hilo bandiko jamani hamkulisoma vizur au mimi peke yangu ndio nimelisoma vibaya?

maana kila mtu anauliza wana makosa gani . wakati kicha cha habari hapo juu na hata habari yenyewe ime ainisha makosa

bas nikiwa kama msomaji mwenzenu labda niwaelekeze tu kwa mujibu wa hilo bandiko kuwa makosa yaliyopelekea wafukuzwe ni

UTORO & KUGUSHI
 
Kwa kosa la kutairiwa wakiwa wakubwa
JamiiForums726260889.jpg
 
Madiwani (std 7) wanafukuza wataalam waliosoma mpk madarasa yamewabomokea
 
Madiwani wana mamlaka gani ya kufukuza waajiriwa ambao wamepewa vibali na taasisi nyingine.

Madiwani ni vyeo vya kisiasa wana uelewa gani juu ya professional. Hii nchi ujinga umezidi sana.

Ndio Yale Yale ya watu 300 pale dodoma kuamua mawazo ya watanzania million 60
 
Back
Top Bottom