Shirika la Afya Duniani imetangaza Idadi ya Vifo vya Ebola kufikia 31 DRC

Shirika la Afya Duniani imetangaza Idadi ya Vifo vya Ebola kufikia 31 DRC

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
1758264101258.png

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa watu 31 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Spetmeba 2025. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, akizungumza jana Septemba 18, 2025 mjini Geneva alitoa taarifa kuwa kuna jumla ya wagonjwa 48 waliothibitishwa na wanaoshukiwa kuwa na virusi hivyo, katika mlipuko wa kwanza baada ya takriban miaka mitatu

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimeeleza wiki iliyopita kuwa ugonjwa huo ambao awali ulikuwa umejitokeza katika wilaya mbili, sasa umeenea hadi wilaya nne. Mlipuko huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza wiki mbili zilizopita karibu na mji wa Bulape.

Tedros amesema WHO na washirika wake wanaendelea kusaidia juhudi za serikali ya Congo kwa kusambaza zaidi ya tani 14 za vifaa tiba na dawa muhimu, pamoja na kutuma wataalamu 48 kusaidia kudhibiti mlipuko huo

Soma pia DR Congo yathibitisha Mlipuko Mpya wa Ebola Kusini mwa Mji wa Kasai, idadi ya Vifo ni 15 hadi sasa

==========

The World Health Organization (WHO) has announced that 31 people have died from Ebola in the Democratic Republic of the Congo this month

WHO Director-General Tedros Adhanom Ghebreyesus told reporters on Thursday in Geneva that there are 48 “confirmed and probable cases” in the DRC amid its first Ebola outbreak in three years. The Africa Centers for Disease Control and Prevention said last week that the disease, previously confined to two districts, has now spread to four

The outbreak was first announced two weeks ago near the town of Bulape

Tedros said WHO and its partners were supporting the government’s response, delivering more than 14 tons of essential medical equipment and supplies and deploying 48 experts


Source: Aljazeera news
 
Back
Top Bottom