Responded Shirika la Bima la Taifa (NIC) hawazingatii Mikataba ya wateja wao, hususani Ajira Mpya

Responded Shirika la Bima la Taifa (NIC) hawazingatii Mikataba ya wateja wao, hususani Ajira Mpya

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
A

Anonymous

Guest
Shirika la Bima la Taifa (NIC) kumekuwa na changamoto kwenye makato kinyume na makubaliano ya wanachama hususani ajira mpya jambo ambalo linapelekea migogoro baina ya Sirika na wateja wake linapokuja suala la kujitoa kwenye huduma.

Elimu inayokuwa ikitolewa haiendani na mambo yanayofanyika baada ya mwanachama kujiunga.

Kwa mfano, mtu anaweza kujiunga Bima ya Maisha ya majaliwa ya miaka 5 kwa yenye thamani ni milioni 2 kwa makato ya elfu 20,000 lakini wao watabadilisha na kutengeneza mikataba yao ambayo ni tofauti na makubaliano ya awali ya wateja.

Wito wangu:
Mamlaka zinazohusika kusimamia mikataba ya wateja wawe na uwazi wakati wa kutoa elimu hususani vyuoni ambapo huko ndo hupata wateja wao.

Pia soma ~ Shirika la Bima la Taifa (NIC): Mteja mwenye changamoto za huduma zetu afike ofisi kwa uchunguzi na ufafanuzi zaidi
 
Back
Top Bottom