Responded Shirika la Bima la Taifa (NIC) wametuunga uanachama bila hiyari yetu na hawataki kututoa

Responded Shirika la Bima la Taifa (NIC) wametuunga uanachama bila hiyari yetu na hawataki kututoa

A

Anonymous

Guest
photo_2026-06-15_16-35-26.jpg
Kero yangu ni kuhusu Shirika la Bima la Taifa NIC (National Insurance Company)... kwanza walipita makazini kutoa orientation jinsi wanavyofanya kazi... baada ya kusaini zile karatasi za mahudhurio waliunganisha baadhi ya watumishi moja kwa moja pasipo kuwauliza na wanawakata kwenye mishahara yao....

Na unapotaka kutoka Wana sababu nyingi za kutokukutoa wanasema mpaka bima ikomae na wale bima zilizokomaaa hawajawahi wapatia kiasi chao.

Hawataki kabisa mtu atoke ukienda halmashauri kuomba utolewa unaambiwa mpaka uende OFISI za NIC ukifika hizo OFISI zao wanakuzungusha tu, hasa kwa mkoa wa simiyu ambayo OFISI zao ziko shinyanga.

Mnisaidie tu kuwasema yamkini watakubali maombi yetu ya kujitoa kwa amani.

Ufafanuzi ~ Shirika la Bima la Taifa (NIC): Mteja mwenye changamoto za huduma zetu afike ofisi kwa uchunguzi na ufafanuzi zaidi

Pia soma: KERO - Shirika la Bima la Taifa (NIC) hawazingatii Mikataba ya wateja wao, hususani Ajira Mpya
 
Usiende kubembeleza halmashauri mwalimu
Anzia TAKUKURU
Then tafuta mwanasheria mpeleke DED mahakamani amekuibia pesa yako ya mshahara.
 
Back
Top Bottom