Shirika la Bima Ya Afya Tanzania (NHIF) linafilisika. Nini kimesababisha haya yote na hatua zipi zichukuliwe kutatua changamoto hii?

Lile ni kwa ajili ya walimu tu na kada za chini walikosea kuinvolve taasisi kubwa zenye package kubwa mfano bot bunge nssf nmb nk
 
Siasa zinaongoza aya mashirika ndio inafata taaluma. Hapo shirika limeshindwa accommodate scope ya watu million 4. Nauliza tukiongezeka tukafika million 10.

Serikali wanadhani kua kuongeza wigo wa watu kutasaidia wao kupata fedha, nadhani dhana yao ni kuwa watanzania wengi hawaumwi.

Watanzania wengi wanaumwa sema wanachofanya ni kumaliza vipimo na dawa kwenye pharmacy. Gharama zitabaki pale pale ata wakifanya bima lazima kwa watu wote.

Serikali ijitathimini, unakuta nhif inashiriki hadi kwenye miradi ya ujenzi, nje kabisa mlengo wa kuanzishwa mfuko huo.
 
Mfuko bado uko imara kuendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya malipo kwa wanufaika wake.
Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa sasa ni wananchi wengi zaidi kujiunga ili kuimarisha zaidi uhai wake.
Mfuko uko imara vipi kama Dispensary hata pain killer tu kama framer haipo kwenye bima? Tube kama volin Dukani ni 2500 lakini dispensary unaambiwa NHIF imeziondowa kwenye orodha, kipimo cha Typhoid hakipo inabidi ulipe cash hivi kazi ya bima ni nini? hivi huko maofisini MNA akili timamu?

Hamjui Dispensary ndio ziko mitaani Kwa wananchi zipewe access kubwa kupunguza mlundikano kwenye mahospitali makubwa?

NHIFTZ usikimbie, tunaomba majibu.
 
Trust me, kwa jinsi nchi hii tulivyo na viongozi majizi, huu mfuko unapigwa vibaya sana na hakuna hatua zozote zinachukuliwa na ndio matokeo ya sekeseke lote hili
 
Nina shaka unachanganya- unazungumzia NHIF au NSSF?
Hata kama nimechanganya mkuu, lkn usilolijua mashirika yote ya bima magu alikomba ela akafanyia yake waliokua wanafanya miradi yao kayasimamisha
 
NHIF Ina mradi gan? Au hujui NHIF Ni nn? Taja mradi mmoja wa NHIF waliokuwa nao.

Au unachanganya na NSSF?

Mwisho lakini si kwa umuhimu, HII ID mpya ulifungua kwa sababu hii?
Lakini ela zilichukuliwa au hazikuchukuliwa?
 
Ushauri wangu, kama Walivyokusudia kuwapa Wastaafu Wazee Mafao Yao kwa Kikokotooo,wakidai Mifuko ya Jamii inakufa. Basi na NHIF watibu Wanachama wao Kwa Kikokotooo. Wapige % za Uchangiaji watibu nazo.
 
Jiwe ndiyo chanzo cha NHIF kufa.
(a) Alikomba fedha zote toka mfuko huu na mifuko mingine
(b) Alilaizimisha kupewa gawio
(c) Zile trilion 1.5 alizokwapua kama mnakumbuka. Sehemu ya fedha hii ilitoka NHIF
 
Jiwe ndiyo chanzo cha NHIF kufa.
(a) Alikomba fedha zote toka mfuko huu na mifuko mingine
(b) Alilaizimisha kupewa gawio
(c) Zile trilion 1.5 alizokwapua kama mnakumbuka. Sehemu ya fedha hii ilitoka NHIF
Huenda hufahamu kitu chochote. Kwa mujibu wa report ya CAG ya mwaka huu pesa ambayo ilichukuliwa NHIF ni ya ujenzi wa hospital ya Benjamin mkapa, ambayo Ni bil 129. Na ndio hadi Leo serikali haikurejesha hiyo pesa. Au unataka kusema report ya CAG ya mwaka huu imempendelea magufuli?
 
Nitachangia kwa haraka namna ya kunusuru NHIF

1. Tehama haijawekwa vizuri - ili ku-control madai, collusion kati ya watoa huduma na NHIF staff; madai yalitakiwa yawe processed 80% electronically na 20% manually.

2. Timu ya wataalam wa TEHAMA wa humu nchini wakusanywe, wapewe exposure hasa South Korea na watengeneze system ya kudhibiti fraud.

3. Siasa iwe mbali na Mfuko; usiwe wa kuwafurahisha wanasiasa (Ministers);

4. Actuarial Dept iimarishwe na actuarial valuation ifanyike kila mwaka na kutoa mwongozo

5. Katika Social Health Insurance kuwa na package tofauti kama Wabunge, BOT, TRA, NMB n.k ni KOSA KUBWA. Makundi hayo yana mishahara mikubwa hivyo walitakiwa wachangie fedha nyingi zaidi na hivyo kuwepo kwa Social Solidarity. Mtu apate huduma bila kujali alichochangia.

6. Serikali itafute maoni ya wenye uzoefu wa SOCIAL Health Insurance na Actuaries watoe maoni yao ya kisayansi sio ya kumfurahisha mtu yeyote.

7. Board inatakiwa iwe na wataalam wa masuala haya na iwatumie kwa hali hii ilikofikia NHIF. SIYO kuishia kufanya ziara mikoani kuelezea Toto Afya Kadi, Vifurushi vya NHIF. Michango inatakiwa izidi malipo ya madai ya watoa huduma,

8. Mfuko ujenge reserve kila mwaka; admin expenses za NHIF ziangaliwe upya;

9. Ajira zinazoweza kufanywa na TEHAMA zifutwe n.k.


 
NHIFTZ chukua hayo madini,kesho Bernard Konga aione mezani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…