Shirika la Life Water lawaondolea wananchi 2,584 adha ya ukosefu wa maji

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Shirika la Lifewater International Tanzania limetekeleza mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Kijiji cha Bugogo, Kata ya Mwamala, wilayani Shinyanga, hatua inayowaondolea wananchi wa kijiji hicho changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo jana, Mkurugenzi wa Lifewater International Tanzania, Devocatus Kamara, amesema mradi huo umenufaisha zaidi ya wananchi 2,584 na umegharimu shilingi milioni 425.1.

"Lengo la mradi huu ni kuwawezesha wakazi wa Bugogo, shule na zahanati kupata huduma ya maji safi na salama ndani ya umbali wa mita 400 kutoka majumbani mwao. Tumefanikisha ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji, hatua inayopunguza muda wa kutafuta maji na kuwawezesha wananchi kutumia muda wao kwa shughuli nyingine za maendeleo," amesema Kamara.

Ameongeza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Agosti 2022 na kukamilika Novemba 15, 2024, kwa kushirikiana na Ruwasa waliochangia shilingi milioni 2.7, huku wananchi wakichangia nguvu kazi yenye thamani ya shilingi milioni 37.5.

Kamara amebainisha kuwa chanzo cha maji katika mradi huo ni kisima kirefu cha mita 115 chenye uwezo wa kutoa maji lita 12,000 kwa saa. Maji hayo yanasambazwa kupitia mtandao wa mabomba wenye urefu wa kilomita 19.479, huku yakihifadhiwa kwenye tangi lenye ujazo wa lita 60,000.

Kwa mujibu wa Kamara, mradi huo sasa unakabidhiwa kwa Chombo cha Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO), ambacho kitakuwa na jukumu la kuendesha huduma za maji na kuunganisha wateja wa majumbani.

Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum, amepongeza shirika la Lifewater International kwa kushirikiana na serikali katika kutatua tatizo la maji safi kwa wananchi wa jimbo lake.

"Mradi huu ni sehemu ya jitihada kubwa zinazofanywa kuhakikisha wananchi wa Solwa wanapata maji. Tunatarajia kukamilika kwa mradi wa Tindepackage, ambapo kati ya vijiji 126 vya wilaya ya Shinyanga, vijiji 109 vitakuwa na maji, huku vikisalia vijiji 17 pekee," amesema Mbunge Salum.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amepongeza Lifewater International kwa kusaidia serikali katika kutekeleza ajenda ya "Kumtua Mama Ndoo Kichwani" inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Mradi huu ni mkubwa sana na una umuhimu mkubwa kwa wananchi. Nawapongeza wadau wa maendeleo kwa kuwekeza katika miradi ya maji ambayo inasaidia kuboresha maisha ya watu, hususan wanawake na watoto," amesema Mtatiro.

Ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha huduma ya maji safi inawafikia wananchi wengi zaidi.
Baadhi ya wakazi wa Bugogo, akiwemo Flora Masanja, wamesema mradi huo umewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, hali ambayo hapo awali ilisababisha hasara kwa kupoteza muda mwingi badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Katika hafla hiyo, Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum, aliwakabidhi rasmi Hati ya Makabidhiano ya mradi huo kwa Chombo cha Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO), ambacho kitakuwa na jukumu la kuendesha na kusimamia mradi huo kwa manufaa ya wananchi.
 
Kazxi nzuri sana hongera sana Life water International
 
Back
Top Bottom