Shirika la Ndege la Ethiopia limenifanya nateseka

Shirika la Ndege la Ethiopia limenifanya nateseka

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,465
Wandugu,

Nilimaliza chuo mwaka 2012 baada tu ya kumaliza chuo nilikuwa na Akiba yangu ya 2ml. Nikaamua kufanya biashara ya simu.

Miaka miwili baadaye nikafanikiwa kuwa na mtaji, nikaamua kukopa benki Kwa kutumia hati ya Miami.

Ule mkopo nikaamua kwenda kufungashia Dubai, Kwa msaada wa Rafiki yangu fulani nikafanikiwa kwenda na kurudi salama.

Sasa Wakati wa kurudi pale Dubai Kwenye ukaguzi nikapita bila Kufika mlangoni nikakuta Wahudumu wakasema tusiingie na mizigo ndani, sikubisha mim na wengine tukakabidhi mizigo.

Sasa safari ikaanza, Kufika Bongo mizigo haipo Kwenye mkanda, wakasema umebaki Dubai. Wakasema utakuja na ndege inayofuata.

Wandugu hadi leo tangu tarehe 29/3/2014 nilipata mwanasheria kila siku ni maneno hakuna mizigo nimebaki na vijikaratasi.

Napambana kulipa mkono hadi leo Sina msaada.

Kama Kuna anayeweza kunisaidia please wapendwa nimerudi nyuma Sana, nimevunjwa ndoto Zangu, mzigo ulikuwa memori card ELFU 10,nyingi Zilikuwa na oda milioni zaidi ya 50 zimepotelea mikononi mwa kampuni hii kubwa ya ndege.
 
Pole mkuu, jaribu kwenda wizara ya mambo ya nje kitengo cha malalamiko wanaweza kukusaidia
 
Wao wamekiri kuwa mzigo waliupokea? Documents zote za manunuzi unazo?
 
Wamekiri, nina kile kikaratasi tu cha mzigo na tickets, risiti zilikuwa kwenye hilo begi ndugu yangu
 
ulikuwa unawakilishwa na Mwanasheria mwenye Reputation gani???

kwasababu kama una Kila kitu ambacho kinaonyesha Mizigo ulikuwa nayo na ilipotea kwa uzembe wa hilo Shirika, ungekuwa umeshapata Mizigo/Compasation zako kipind hicho hicho!!!

Tafuta Reputable Law Firm ikusaidie!!!!!

Sikushauri uende wizarani/serikalini kuwasilisha hilo tatizo lako, Utapoteza muda wako TU!!
 
Na kila wakiulizwa wanasema upo ethiopia wanautafuta nilikata tamaa zaidi Kwasababu NILIKATA JAMAA MWANASHERIA WA KAMPUNI INAITWA MROSO IPO DAR NA ARUSHA, AKANIAMBIA KWAKUWA SINA HELA ATANISAIDIA ILA ATADAI 100ML PAMOJA NA USUMBUFU, WANDUGU KWELI, SIKUWA TENA NA KITU ADI LEO JAMAA HAPOKEI SIMU YANGU
 
Wamekiri, nina kile kikaratasi tu cha mzigo na tickets, risiti zilikuwa kwenye hilo begi ndugu yangu

Ok, wamekiri kupokea beg with vitu vyote vilivyomo ndani? Inshu ni kuthibitisha kuwa ndani kulikuwa na mzigo wa that amount, tho bado wana makosa, in waste scenario ni kwenda dubai na kutafuta copy za risit, kwa maana beg laweza kuja limejazwa nguo tu!! Pia scaning ya dat date inaweza onyesha ulibeba nini, hyo watakulipa, na pesa ya riba ya biashara ambayo ilitakiwa kufanyika mwaka mzima, nenda wizarani kama jamaa alivyosema hapo juu, ila mashirika ya ndege hayana chombo inayoyadhibiti kisheria? Kwenye swala la kulinda wateje, Wadau wajibu, tupate kwa kuanzia
 
kama unadocument zote za mzigo ,busara tafuta mwanasheria anaejielewa mfile kesi,

Basi siku nyingine weka hata hyphen m-file badala ya 'mfile' maana inasepetuka na kuleta maana tofauti mukulu😀
 
Fungua kesi hapo lazima uwe milionea voz itabidi ulipwe hadi psychological tocha. We mkomalie mkurugenzi wa shirika hilo
 
Kuna jamaa hivyo hivyo kwenye rwandair alipoteza mzigo zaidi ya miez mitatu ikapatikana alilipwa vizur mno
 
Daah, hii inshu inabidi wataalam wa mambo waje hapa kusaidia ushauri, imeniuma sana aisee, na nimejifunza kitu!! Docs inabidi kutembea nazo kwenye beg ya mkononi
 
Ndugu napambana na deni crdb, kwenda dubai Wakati huu ni taabu sina Tena uwezo, nalinda wasiuze nyumba ya mzee akapata presha Kwa ajili yangu,
Wandugu huko serikalini waliopewa dhamana wana njaa Sana nahisi Ata mwanasheria yule Alihongwa naogopa Sana Kwa Sasa sijui mtu swahili wa kunisaidia
 
Kama hali yako ni ngumu kiasi hicho nenda kituo cha sheria na haki za binadamu watakusaidia bureeee tena wana wanasheria mahili
 
Pole sana ndugu yangu.
siku zote unatakiwa ujue kuwa bag la kuingia nalo ndani linatakiwa lisiwe kubwa sana kwa size na uzito kama 15kgs; Na ni vizuri lisiwe na vitu kama battery, vimiminika, mikasi, wembe nk.

kama begi lako ulirudishwa nalo mlangoni sina hakika kama liliweza kusajiliwa na kupewa luggage tag number? kwani kama hujapewa hiyo ref namba, mzigo huenda kuishia kwenye Godown ya hiyo ndege kama unidentified baggage.

-Kama bag lako lilipokelewa na ukapewa tag/ tag number; na ulipofika Bongo ukajaza lost luggage form kwa ref ya hiyo tag number ilikuwa rahisi kulifuatilia kwa wakati huo huo; naona umechelewa sana kuleta hapa

Haya mashirika ya ndege yapo covered nakumbuka mzigo ukipotea mikononi mwao yanaweza kulipa sina hakika vizuri ila nafikiri ni maximum ya 5M zaidi ya hapo unadai kwenye insurance yako kama unayo
 
Inauma sana. Ndoto zinazimika kama Mshumaa.

Pole sana. Hope wajuzi wa hapa Jukwaani watakupa msaada.
 
Naitaji msaada Sana Sana ktk maelezo yangu sijadanganya neno sijui cha Kafanya hakika
 
Kwenye ukaguzi nikapita bila, Kufika mlangoni nikakuta Waudumu wakasema tusiingie na mizigo ndani, sikubisha mimi, na wengine tukakabidhi mizigo,

Hapo ndo ulipo ugumu wa kesi yako
Kwa uzoefu wangu mdogo, napata picha kwamba huo mzigo wako ulikuwa si wa ku-check-in kwa maana ya kuwakabidhi, bali ulikuwa ni hand luggage kwa maana unaruhusiwa kuingia nao ndani ya ndege.

Sasa wale wahudumu walipokuzuia kuingia nao sidhani kama walikupa risiti ya kuonyesha umewakabidhi huo mzigo, sana sana watakuwa waliweka stika ya kuonyesha wapi mzigo utashushwa (destination)

Najaribu tu kufikiria lakini
 
Back
Top Bottom