esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
WAKATI serikali ikisema inatenga Sh bilioni 500 ii kuendelea kuboresha utendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kampuni hiyo kwa sasa inamiliki soko la usa ri wa anga la ndani kwa asilimia 40.8 kutoka asilimia 2.5 za mwaka 2017.
Aidha, ATCL imeongeza idadi ya abiria kutoka 216,798 katika kipindi ha Julai 2017 hadi Machi 2018 kukia abiria 307,192 waliosarishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2018/2019 hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 41.69.
Akihutubia Bunge kuomba fedha za bajeti kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri Isack Kamwelwe alisema Sh milioni 500,000 zilizotengwa zinakusudia kukamilisha malipo ya ndege ya pili aina ya Boeing 787 Dreamliner na ndege ya nne aina ya Bombardier Q400. Pia alisema fedha hizo zitatumika kufanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya A220- 300; ununuzi wa ndege moja aina ya Bombardier Q400 na kuendelea kuboresha karakana ya matengenezo ya ndege iliyoko KIA na kulipia madeni yaliyohakikiwa na gharama za kuanzia kwa ndege mpya zitakazopokelewa katika kipindi hicho.
Kamwelwe alisema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 serikali ilipokea ndege tatu mpya ndege, moja ikiwa ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba abiria 262. Huku ndege mbili za masafa ya kati zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zikiwasili Desemba 2018 na Januari 2019.
Alisema ongezeko hilo la ndege limesababisha ATCL kutoa huduma za usari katika vituo tisa vya ndani ya nchi na vituo vitano vya kikanda. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Dodoma, Mbeya na Zanzibar.
Vituo vya kikanda ni Entebbe, Uganda; Bujumbura, Burundi; Harare, Zimbabwe; Lusaka, Zambia na Hahaya, Comoro. Aidha, alisema ATCL inatarajia kuanza kutoa huduma za usari wa anga katika mji wa Bangkok, Thailand; Mumbai, India; Johannesburg, Afrika Kusini na Guangzhou, China.