Shirika la Posta linatumia kigezo gani kutoza pesa?

Shirika la Posta linatumia kigezo gani kutoza pesa?

Azniv Protingas

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2020
Posts
335
Reaction score
554
Nilipokea SMS kuwa nifike posta nikachukue mzigo wangu na pia kuna malipo ya 3000/-.
IMG_20240823_072405.jpg

Mzigo wenyewe hata gram 10 haufiki na hiyo 3000 inakaribia nusu ya gharama ya kununulia bidhaa, pamoja na usafiri mpaka kufika Tanzania.

Mimi nilitegemea mzigo wangu utakuja kwa speedaf kwa sababu nilichagua cainiao economy kwenye shipping pale. Na speedaf inakuwa haulipii tena ukishalipa online.

Sasa kama speedaf wanatoa mizigo airport na wanatufanyia delivery hadi nyumbani kwa bei ileile ambayo tumelipia awali, kwa nini shirika la Posta litutoze pesa na bado mizigo tunafuata wenyewe ofisini.
 
Back
Top Bottom