Shirika la Reli Tanzania (TRC) laomba radhi kutokana na kuchelewa kwa safari kulikosababishwa na changamoto zilizo nje ya uwezo wao

Kila kitu kimepangwa na nani?
Sasa jiulize inakuaje watu wanajua mtu flani atasafiri siku flan kwa gari fulani au atakuwa sehemu fulani wakati fulani.
Hapo ndio ujue wamekaa chini na kupanga ndo mana nasema hakuna linalotokea kwa bahati mbaya, hayo yamepangwa.
 
Mdogomdogo safari ya kwenda kufa Kwa mradi imeanza mwisho wa siku watasitisha huduma na kumpa mwekezaji

Wampe mwekezaji sasa, serikali haiwezi endesha huu mradi. Wakichelewa kuwapa wawekezaji hii treni haimalizi huu mwaka.
 
Hii ni excuse ya kitoto,kama wanajua kumi kupishana kwa nini wasipange ratiba vizuri?.. kupishana watu wamesubiri kwa saa nne na zaidi!!
Siyo kweli mkuu, hii ni sababu ya kutunga tu.
 
Ili kuondoa hili tatizo waongeze station. Eg kati ya morogoro na Ngerengere. Station ya mikese iongezwe
 
Kwenye kusubiria Treni kupishana kuna uzembe unafanyika,hii sio mara ya kwanza kulisikia hili,fanyeni hesabu zenu za masaa vizuri,inawezekana hao mastation master kwa sababu za uoga wanaweka Treni moja muda mrefu ikisubiria nyingine bila sababu ya msingi wakati inawezekana bado iko mbali...
 


Tatizo la Tanzania wahujumu wa mashirika ndiyo viongozi wa hayo mashirika. TRC inahujumiwa na wenye mabasi na hilo liko wazi. Kila siku tutasikia hitilafu mpaka abiria wapungue mtandao mzima hauna tatizo lolote ni matatizo ya kutengenezwa
 
Treni ya Mwendokasi inayofanya safari zake Dar es salaam - Dodoma
sababu ya kusimama huko ni pamoja na kusubiri kupishana na treni iliyokuwa ikitoka Dar es salaam kuelekea Morogoro! Treni zote zinaelekea upande mmoja, ya kwanza inakwenda Dodoma na yapili inakwenda Morogoro, inakuwaje ya Dodoma isimame kuipisha ya Morogoro! Inamaana ya Morogoro ina kasi zaidi ya ile ya Dodoma? Na iweje hili liwe nje ya uwezo wenu?
Hebu wekeni sawa hili ili liingie akilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…