Treni ya shirika la reli tanzania imekwama eneo la same toka jana asubuhi. Treni hiyo iliyoondoka dar juzi kwenda mikoa ya kilimanjaro na arusha ilitegemewa kuwasili kilimanjaro jana alfajiri ila imekwama maeneo ya same pasipo shirika la reli kutoa taarifa kwa uma au abiria huku wananchi wakiendelea kuteseka maporini. Baadhi ya abiria wakiwemo watoto na wagonjwa imewabidi kukodi pikipiki iwapeleke same mjini ambapo ni umbali mrefu ili waweze kuendelea na safari zao. Shirika limeshimdwa kuwa na uungwana angalau kwa dharura kuhakikisha wateja wao wanasaidika. Serikali ya Mama kizimkazi imekwama kwa kila kitu.