Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Wanawadanganya watu etioooo tumejenga miundo mbinu mara ooo hiki na kile.

Hizo pesa zilizo jenga hiyo miradi ni kodi za watanzania. Hakuna aliye tumia fedha yake ya mfukoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani kama kungekuwa na uwezo tukatolewa woote tukashushwa pale Ulaya tukaishi kwa siku moja halafu turudishwe hapa wallah mabadiliko yangefanyika kwa siku moja manake naona watu wameishi maisha ya leo afadhali ya jana mpaka wamekuwa chanda na pete kama mateja vile
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.

TBC nao wametumwa nini? Mlikataa kurusha matangazo kwa vyama vya upinzani kwa muda mrefu tu, mling'ang'ania ccm tu. Malalamiko yalipozidi mlijitetea kwamba vyama vingine havifuati utaratibu ikiwemo kuwaalika katika shughuli zao. Sasa leo hamja alikwa mmekuja wenyewe na wenye mkutano wamekataa, nini kinawafanya mlalamike? Eti si uungwana na kunahatarisha usalama wa watendaji na vifaa, si mseme moja tu hamkutegemea hilo labda mlidhani watawashangiria kwa unafiki wenu. Kama mlitumwa kutafuta sababu basi mmeipata haya nendeni polisi na tume ya uchaguzi. Na wasivyokuwa na aibu utasikia matamko yatakavyo pishana kila kona.
 
Bora waache tutakuja kuelewana tu nao baada ya uchaguzi. Vijana sommeni sana tasnia ya habari huku naona nafasi zitapatikana sanna
 
Sasa ukishalima huko bila ya access ya barabara, madaraja na train nani atakuja kufuata hizo bidhaa huko.

Uchumi sio swala la kuku na yai kipi kimetangulia; serikari inahitaji kutengeneza mazingira kwanza yanayoweza chochea wafanyabiashara kuchangamkia fursa za uchumi.
Hapo ni tatizo siwezi kubisha hii biashara ya wakurugenzi kunyima wapiga kura haki ya kuchagua kwakweli sio democracy.

Ningelikuwa mimi ndio Kiongozi upinzani sasa hivi nipo mahakamani naomba NEC isitishe zoezi la uchaguzi mpaka hilo jambo likae sawa, but thats just my thinking.

Na wewe Kilatha naona akili inaanza kukurejea MATAGA wewe. Binadamu yeyote anayependa HAKI hawezi kufurahia uhuni huu wa CCM kuengua wagombea wa upinzani, bila kujali itikadi ya chama. Lazima tuwe na ubinadamu
 
Sasa ukishalima huko bila ya access ya barabara, madaraja na train nani atakuja kufuata hizo bidhaa huko.

Uchumi sio swala la kuku na yai kipi kimetangulia; serikari inahitaji kutengeneza mazingira kwanza yanayoweza chochea wafanyabiashara kuchangamkia fursa za uchumi.
Hicho kilimo cha mkono au kilimo kipi hilo soko la nje umewatafutia unataka kujifunza kilimo jomba sogea hapo jirani tu kwa swahiba wala sio mbali
 
hao masikini waliojaa ccm ndio ushindi wa chama matajili wenu wana wanufaishaje.
Tutanufaikaje wakati masikini wajinga ndio wanasababisha hali hii
Hadi pale mtakapokua matajiri wa akili ndio tutanufaika
 
[emoji837] Alert

CHADEMA hakikisheni kesho Lissu hashiki simu yake siku nzima. Asije akaona Umati wa Magufuli, Viwanja vya Jamhuri Dodoma, akaanza kuleta story za kujitoa kwenye Uchaguzi. Hakuna mtu kujitoa uchaguzi huu, kesho kazi inaanza. Karibuni Jamhuri
Wanaenda kushangaa wanamuziki na wakina shilole weka akilini na sii vinginevyo
 
Yaani kama kungekuwa na uwezo tukatolewa woote tukashushwa pale Ulaya tukaishi kwa siku moja halafu turudishwe hapa wallah mabadiliko yangefanyika kwa siku moja manake naona watu wameishi maisha ya leo afadhali ya jana mpaka wamekuwa chanda na pete kama mateja vile
Yaani wana ccm wanaishi maisha ya mlevi wa gongo maana kila akinywa lazima afumbe macho kwa uchungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bado sija kuelewa hapo huja elewa nn[emoji846][emoji846][emoji846]
Sasa kama hauna ubongo utaelewaje?
tapatalk_1592766000193.jpg
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.

TBC kabla ya sijui Kukimbilia Polisi na kutaka muhakikishiwe Usalama 'Mjitathmini' je, na nyie 'Mkishtakiwa' kwa Mwenyezi Mungu mtapona kweli?
 
Elimu ya Tanzania ni kwa ajira tu, haisaidii mtu kwa namna nyingine akiwemo Director Ayoub
Huyu huwezi kuamini ni yeye, na kwamba, eti hajui kwanini kuna chuki kubwa ya jamii dhidi ya TBC

1. Hiki ni chombo cha CCM na Watawala na hakiwezi kutenda haki bila ubaguzi. Hivi Ryoba anaweza kusema nini kama mkurugenzi tu wa shirika? Kama Tido alitendwa nani anayeweza tena.

2. TBC walichokifanya kwa CDM ilikuwa ni upuuzi !!
kama wanalinda maadili ya Taifa mbona kila siku Wanawake na Akina Mama wanadhalilishwa na hatujawahi kuona wanakata matangazo. Hivi Ayoub hayaoni hayo. Shame on you

3. TBC Wangekuwa na uwezo mzuri wa kufikiri wangekaa kimya.
Hili ni sawa na kutaka huruma za umma kwamba majambazi waliingia kwangu na kisha ''wakamkamata mke n.k.''
Kila mtu sasa anauliza nini kilitokea na hata waliokuwa hawana habari sasa wanayo

Ukiwa msomi wa Tanzania uwe profesa au Mkurugenzi , moja ya maadili ya kazi 'ni kufungia akili kabatini'' na kukubali kupokea maagizo kutoka majuu. Shame on you!

Pascal Mayalla Mag3 JokaKuu
 
Back
Top Bottom