Shirika la WAICO kuleta mapinduzi makubwa kwenye utawala wa AI duniani

Shirika la WAICO kuleta mapinduzi makubwa kwenye utawala wa AI duniani

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111654823324.jpg


Julai 16 mwaka 2026, ni siku adhimu ambayo imeingia kwenye vitabu vya historia, baada ya China kuandaa hafla ya kusaini mkataba wa kuanzishwa kwa Shirika la Ushirikiano wa Akili Bandia Duniani (WAICO) huko mjini Shanghai. Nchi 29 zikiongozwa na China walisaini makubaliano hayo kama wanachama waanzilishi.

Hii ni hatua kubwa kwa China kuitikia wito wa nchi za Kusini mwa Dunia na kuunganisha jumuiya ya kimataifa katika kuhimiza kwa nguvu zote maendeleo na utawala wa AI duniani. Pia ni hatua muhimu katika historia ya maendeleo ya AI.

Tukio hili kubwa la kupigiwa mfano pia linaonesha nafasi ya China inavyobadilika katika utawala wa kisayansi duniani. Kwa sasa China sio mfuasi tena wa sheria za kimataifa, bali inatumia uwezo wake wa uvumbuzi na utawala wake bora kubeba jukumu linalozidi kuwa kubwa katika kuunda sheria za kisayansi duniani.

Ni dhahiri kwamba China sasa ni miongoni mwa viongozi wa dunia katika uwanja unaoendelea kukua kila siku wa AI. Kwa mtazamo wa nguvu ya kiteknolojia, China inaongoza duniani kwa idadi ya maombi ya hataza za AI na machapisho ya utafiti, huku upakuaji wa mifumo yake mikubwa pia ukishika nafasi ya kwanza duniani. Kwa upande wa utawala wa AI, China inaendelea kukuza teknolojia kwa matumizi mema kupitia mbinu jumuishi ya hatua ndogo lakini za haraka.

Kama kiongozi wa AI duniani, China imeendelea kuimarisha na kupanua ushiriki wake katika utawala wa AI duniani. Imeweka mbele Mpango wa Utawala wa AI Duniani, Mpango wa Utekelezaji wa Kujenga Uwezo wa AI kwa matumizi mazuri na kwa wote na Mpango wa Ushirikiano wa Kimataifa wa AI+.

Mbali na kutoa mipango hiyo, China pia imekuwa ikiendelea kutoa suluhu kwa maendeleo ya kimataifa katika zama za akili bandia kwa vitendo halisi. Kuanzishwa kwa WAICO, ni moja ya mifano mizuri na ishara ya kwamba China imetoka kwenye kutetea mawazo hadi kujenga majukwaa na kuimarisha mifumo ya kitaasisi, ikipiga hatua mpya katika mchango wake wa utawala wa AI duniani.

Ni muhimu kuelewa kwamba nchi za Kusini mwa Dunia bado hazijawakilishwa kikamilifu katika mfumo wa sasa wa utawala wa AI duniani. Kwa mujibu wa ripoti ya 2024 ya Baraza la Ushauri la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Akili Bandia, nchi 118 hasa za Kusini mwa Dunia, hazishiriki katika mipango saba ya utawala wa AI isiyo ya Umoja wa Mataifa.

Mifumo ya utawala wa AI iliyopo, kwa kiasi kikubwa imeundwa kulingana na mahitaji ya nchi zilizoendelea na haijafanya mambo mengi ya kushughulikia masuala yanayohusu Kusini mwa Dunia, kama vile mgawanyiko wa AI na uhaulishaji wa teknolojia jumuishi.

Kwa mtazamo huu, kuanzishwa kwa WAICO ni hatua muhimu inayoziba pengo kubwa na kuweka upya vibainishi vya utawala wa AI duniani. Kwa kuanzisha jukwaa wazi linaloondoa mgawanyiko wa kiitikadi na vikwazo vya kiteknolojia, itasaidia kuhakikisha kwamba nchi za Kusini mwa Dunia zinaweza kufaidika kwa usawa na wimbi la uvumbuzi wa akili bandia.

Kutoka uanzishaji wa mifumo mikubwa kama DeepSeek, hadi usaidizi wa China kwenye ujenzi wa kituo cha kompyuta kubwa nchini Zimbabwe na utumiaji wa MAZU; mfumo wa tahadhari ya hali ya hewa unaoendeshwa na AI, suluhu za China sasa zinasaidia katika zaidi ya nchi 40 za Kusini mwa Dunia kuziba pengo la teknolojia. Na WAICO itatoa jukwaa zaidi la kitaasisi kwa teknolojia za China kuzijengea uwezo nchi za Kusini mwa Dunia.

Akili bandia (AI) si hifadhi ya nchi chache teule, na utawala wake wa duniani wala haupaswi kuundwa na nchi chache tu. Hivyo kuanzisha mfumo huu mpya wa utawala jumuishi unaohusisha wadau wengi, hakika itafungua mlango mpya kwa nchi za Kusini mwa Dunia hasa za Afrika ambazo mara nyingi zimekuwa zikitengwa kwenye uanzishaji wa mifumo mikubwa duniani.

Ushirikiano huu utashuhudia ukiinua pakubwa nchi nyingi za Afrika, kwani kati ya wanachama 29 waanzilishi wa shirika hili la WAICO, 10 ni nchi za Afrika, zikiwa ni pamoja na ni Algeria, Cameroon, Jamhuri ya Congo, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Msumbiji, Senegal, Afrika Kusini na Zambia.
 
Back
Top Bottom