Shirikisho la Mpira Uganda (FUFA) laitanganza Express FC kuwa mabingwa kutokana na ligi kusimama kwa Covid-19

Shirikisho la Mpira Uganda (FUFA) laitanganza Express FC kuwa mabingwa kutokana na ligi kusimama kwa Covid-19

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1625117975489.png

Shirikisho la Chama cha Soka la Uganda limemaliza Ligi Kuu ya 2020-21 na kutangaza Express FC kama mabingwa.

Fufa imelazimika kuchukua uamuzi kufuatia tangazo la hivi karibuni la Rais Yoweri Museveni kupiga marufuku shughuli zote za michezo nchini humo kwa sababu ya kuwapo kwa idadi kubwa ya maambukizo ya Covid-19.

Fufa sasa imethibitisha kuwa wameamua kusimamisha ligi hiyo na kuwatangaza timu ya Express FC kama mabingwa kwa sababu ndio waliokuwa juu ya msimamo.

Kwa msingi huo timu hiyo itaiwakilisha Uganda katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika huku URA iliyoshika nafasi ya pili itashiriki kombe la Shirikisho.
 
Kwani ligi nayo kama yetu??

Hadi leo bado?😂
 
Waje wamalizie kukipiga huku Bongo Corona ishatepeta muda sasa.
 
Back
Top Bottom