Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limeahirisha tena kuanza kwa msimu wa 2026/27 wa FKF Premier League, ambao ulikuwa uanze leo Jumamosi, Septemba 19, 2026.
FKF iliwasilisha taarifa kwa wenyeviti na maafisa wakuu wa vilabu Ijumaa usiku, ikisema ligi imesitishwa hadi taarifa zaidi itakapotolewa.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya maagizo mawili tofauti ya Mahakama Kuu za Murang’a na Kiambu kuhusu muundo wa ligi hiyo.
Mahakama ya Murang’a imezuia kuanza kwa msimu hadi mechi ya mchujo ya kupanda na kushuka daraja kati ya Kariobangi Sharks na Mombasa United ichezwe.
Wakati huo huo, Mahakama Kuu ya Kiambu imeagiza FKF kumjumuisha Mombasa United katika msimu wa 2026/27 kama klabu ya 18.
Hali hiyo imevuruga maandalizi ya vilabu ambavyo tayari vilikuwa safarini kwa mechi zao za kwanza. Shabana FC walikuwa Kirinyaga kwa ajili ya kukutana na Posta Rangers, huku APS Bomet wakiwa Nairobi kucheza dhidi ya Mathare United.
Kwa sasa, FKF haijatangaza tarehe mpya ya kuanza kwa ligi, huku vilabu vikisubiri mwelekeo mpya kutoka kwa shirikisho na mahakama.
Source: Easleighvoice.co.ke