SI KWELI Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kuwasajili Wachezaji wa Tanzania bara kama Wageni

SI KWELI Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kuwasajili Wachezaji wa Tanzania bara kama Wageni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Salaam ndugu zangu,

Nimepata taarifa kwamba Shirikisho la soka nchini Zanzibari limeweka ugumu kwa wachezaji wa Tanzania Bara na itawasajili kama Wageni. Taarifa hii imeandikwa:

1693248595673.png

Bodi inayosimamia Ligi kuu ya Zanzibar (PBZ) imepitisha kanuni mpya za Usajili kuwa Klabu yoyote itakayomsaini mchezaji kutoka Tanzania bara ataingizwa kwenye system kama Mchezaji wa kigeni kwa maana lazima akatiwe Kibali cha kuishi Zanzibar ambacho kina gharimu pesa za kitanzania laki 5.

Pia kwenye klabu Moja hawatakiwi kuzidi wachezaji 9

Kwa ligi ngazi ya Mkoa Mchezaji kutoka Tanzania bara atakatiwa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa msimu. Mmoja ambacho kita gharimu Pesa za kitanzania Laki 3.

Kwa upande wa Tanzania Bara, mchezaji akisajiliwa kutoka Zanzibar anahesabika ni mzawa.

Je hii inatengeneza Usawa wa ajira ama Ubaguzi wa Ajira ? Au lengo ni nini ?


Hii kitaalamu inakuwaje kwa kanuni mpya hizo kwa msimu huu wa 23/24 zimeanza kazi.

Kuna ukweli wowote kuhusu hili?
 
Tunachokijua
Mnamo Agosti 27, 2023 kulizuka taarifa katika mitandao ya kijamii zilizoihususha Bodi inayosimamia ligi ya Zanzibar (PBZ) na Shirikisho la soka la Zanzibar (ZFF) kupitisha kanuni mpya za usajili katika vilabu vya soka vya nchi hiyo huku wakidai kuwa Wachezaji watakaosajiliwa kutokea Tanzania Bara watasajiliwa kama Wachezaji wa Kigeni. Taarifa hiyo pia ilidai kuwa Watanzania wakisajiliwa watapaswa kukata vibali vya kuishi nchini Zanzibar. Taarifa hiyo iliyosambaa ilibeba kichwa ilibebeba kichwa ZFF waweka ngumu kwa wachezaji kutoka Tanzania Bara.

Upi ukweli kuhusu jambo hili?

JamiiForums imepitia katika kurasa rasmi za Shirikisho la Soka la Zanzibari (ZFF) na kukatana na kanusho la Taarifa hiyo ambayo imesambazwa. Katika ukurasa wao wa Instagram ZFF wameweka andiko hili:

1693249622328-png.2731914

1693249641456-png.2731915

Hivyo, kutokana na kanusho hilo kutoka kurasa rasmi za ZFF taarifa zinazoenea kuhusu Wachezaji wa Tanzania Bara kusajiliwa Zanzibar kama Wageni hazina ukweli.
Sauti kutoka ndani inaniambia "funga bakuli lako, utazua taaruki"...

Mimi naitii hii sauti..

Ila hii nchi ni ngumu sana..
 
Back
Top Bottom