Shitukeni SUA hawauzi miche ya matunda ni wahuni wanatumia jina la SUA

Shitukeni SUA hawauzi miche ya matunda ni wahuni wanatumia jina la SUA

Jambo ambalo angetueleza ni ikiwa hiyo miti haitowi matokeo sahihi, Lakini hoja ya kuwa miche ilifika haifai hilo halihusiani na mzalishaji bali msafirishaji. Mimi niliagiza hiyo hiyo miche baada ya kuipanda mwaka wa kwanza tu mwembe ulitoa mbegu bila kuzaa, mwaka wa pili ukazaa maembe na mpaka sasa unazaa. hivo ikiwa ulitoka ama haukutoka SUA hoja inakuwa imekufa
Mkuu watu wanaongea kujifurahisha. Njombe mbeya nk kupata miche ya avocado iliozalishwa toleo la kwanza au pili haipo. Kinachofanyika ni kuendeleza miche ilioletwa na wazungu zamani.
Hao SUA sijui wanafanya nini, hakuna sababu ya kuwalaumu vijana wanaochukua vikonyo miche ya zamani na kupandikiza. Hakuna bwana shamba yoyote yule mwenye kitalu chenye vikonyo vya f1 au f2, f3. So hakuna haja ya kuwalaumi hao vijana maana waliopewa dhamana hamna wanachofanya.
Serikali haichukui hatua kuleta vikonyo vipya kilichopo ni kulaumu vijana wasio na elimu ya kilimo.
 
SUA inazalidha wasomi feki!
Inazalisha Tena Miche ya matunda feki????
 

Attachments

  • images (93).jpeg
    images (93).jpeg
    38.2 KB · Views: 6
 
Tatizo theory sana na slide ndo practical pale sua inatakiwa umeze na upige msuli sana ila usipojiongeza kujinoa kwenye vitendo itakuwa ni shida sana . Si ni kweli wazee wa simbi
 
Tayari SUA wameshatekeleza wajibu wao wa kuwapatia elimu hao unaowaita matapeli,
Ungetueleza umepata changamoto Gani kutoka kwa hiyo mzalishaji aliekuuzia Miche ili tujue tatizo ni Nini mkuu
 
Tuachane na hayo, je hiyo miti ukipanda inakubali au haikubali??
Iwe inapakubali au haikubali, kutumia jina la institution kama SUA kunadi miche unayouza ni utapeli. Hata kama hiyo miche ingetoka Holland na iwe na ubora wa kimataifa. Huwezi kuuza bidhaa kwa udanganyifu.
 
Tayari SUA wameshatekeleza wajibu wao wa kuwapatia elimu hao unaowaita matapeli,
Ungetueleza umepata changamoto Gani kutoka kwa hiyo mzalishaji aliekuuzia Miche ili tujue tatizo ni Nini mkuu
Watanzania mbona akili zetu zimekaa kitapeli tapeli tu? Kupata changamoto tu ndiyo tatizo? Kama hao wauzaji wanajiamini ni kwa nini wanatumia jina la SUA? Kwa nini wasiwe wakweli kuwa wamepata elimu kutoka SUA na siyo kuwa miche ni ya SUA?
 
Watanzania mbona akili zetu zimekaa kitapeli tapeli tu? Kupata changamoto tu ndiyo tatizo? Kama hao wauzaji wanajiamini ni kwa nini wanatumia jina la SUA? Kwa nini wasiwe wakweli kuwa wamepata elimu kutoka SUA na siyo kuwa miche ni ya SUA?
Watakuwa SUA wanajua,wangewakanusha kuwa hawahusiki na hawawafahau, watakuwa wamepatavElimu kwao .
 
Mkuuu. Hebu ifike mahala muanze ku appreciate kazi na ubunifu wa watanzania wenzenu. Angeuza mzungu mchina au mwarabu usingeleta daught.
Kama SUA wameshindwa kazi yao walioaminiwa kwa nini usiwapongeze watu wanaowasaidia kufanya kazi yao hao SUA.
Nimewahi andika humu kuwa SUA ni taasisi isio na faida kwa nchii. Mimi ni mkulima wa miti. Viazi mviringo na matunda. Sioni wala sitambui mchango wa SUA na products zao(extension officer), hawana msaada wowote kwa wakulima.
Ninaishi vijijini, kama kuna mtu yupo au kijiji kimenufaika na uwepo wa SUA wajitikeze. SUA kazi yao kubwa ni kijitetea tu, hawanaga jipya.
Mimi nawapongeza vijana walioamua kuwasaidia watanzania.
Ukienda Njombe,Mbeya,Iringa watu waliosaidai sekta ya Avocado ni hao vijana unaowapiga vita.
Ingefaa sana hao SUA kuwasapoti hso vijana si kuwapiga vita. SUA hawawezi kuzalisha miche Tanzania nzima hawawezi, lazima watrain vijjana maana products zao hawana ubunifu wowote huku mtaani wanadai hela za sindano tu.
SUA lazima ijitasmini .
Kijiji chao pendwa ni Mgeta
 
Mkuu embe sh ngapi?
 
Back
Top Bottom