Shitukeni SUA hawauzi miche ya matunda ni wahuni wanatumia jina la SUA

Mkuu watu wanaongea kujifurahisha. Njombe mbeya nk kupata miche ya avocado iliozalishwa toleo la kwanza au pili haipo. Kinachofanyika ni kuendeleza miche ilioletwa na wazungu zamani.
Hao SUA sijui wanafanya nini, hakuna sababu ya kuwalaumu vijana wanaochukua vikonyo miche ya zamani na kupandikiza. Hakuna bwana shamba yoyote yule mwenye kitalu chenye vikonyo vya f1 au f2, f3. So hakuna haja ya kuwalaumi hao vijana maana waliopewa dhamana hamna wanachofanya.
Serikali haichukui hatua kuleta vikonyo vipya kilichopo ni kulaumu vijana wasio na elimu ya kilimo.
 
SUA inazalidha wasomi feki!
Inazalisha Tena Miche ya matunda feki????
 
Attachments

  • images (93).jpeg
    38.2 KB · Views: 6
 
Tatizo theory sana na slide ndo practical pale sua inatakiwa umeze na upige msuli sana ila usipojiongeza kujinoa kwenye vitendo itakuwa ni shida sana . Si ni kweli wazee wa simbi
 
Tayari SUA wameshatekeleza wajibu wao wa kuwapatia elimu hao unaowaita matapeli,
Ungetueleza umepata changamoto Gani kutoka kwa hiyo mzalishaji aliekuuzia Miche ili tujue tatizo ni Nini mkuu
 
Tuachane na hayo, je hiyo miti ukipanda inakubali au haikubali??
Iwe inapakubali au haikubali, kutumia jina la institution kama SUA kunadi miche unayouza ni utapeli. Hata kama hiyo miche ingetoka Holland na iwe na ubora wa kimataifa. Huwezi kuuza bidhaa kwa udanganyifu.
 
Tayari SUA wameshatekeleza wajibu wao wa kuwapatia elimu hao unaowaita matapeli,
Ungetueleza umepata changamoto Gani kutoka kwa hiyo mzalishaji aliekuuzia Miche ili tujue tatizo ni Nini mkuu
Watanzania mbona akili zetu zimekaa kitapeli tapeli tu? Kupata changamoto tu ndiyo tatizo? Kama hao wauzaji wanajiamini ni kwa nini wanatumia jina la SUA? Kwa nini wasiwe wakweli kuwa wamepata elimu kutoka SUA na siyo kuwa miche ni ya SUA?
 
Watakuwa SUA wanajua,wangewakanusha kuwa hawahusiki na hawawafahau, watakuwa wamepatavElimu kwao .
 
Kijiji chao pendwa ni Mgeta
 
Mkuu embe sh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…