Hebu fikiria kwamba, umebaini kuwa shoga yako wa karibu kabisa, ndiye ambaye amekuwa akitembea na mumeo au mpenzi wako. Umekuwa ukimsimulia shida zako na matatizo yako yatokanayo na ndoa yako au uhusiano wenu, yaani mume wako au huyo mpenzi wako kutotulia, ukijua unamsimulia shost wako, wakati ndiye chanzo cha madhila uliyo nayo.
Katika kumsimulia amekuwa akikupa moyo na kukuambia wanaume ndivyo walivyo na wakati mwingine amekuwa akikwambia kwamba, ukiona vipi ni bora uachane naye. Hivi sasa unagundua kwa maumivu kwamba, yeye ndiye ambaye amekuwa akikusababishia maumivu yote. Hebu sema ungefanyaje?