Shoga yako anatembea na mumeo!

Shoga yako anatembea na mumeo!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu fikiria kwamba, umebaini kuwa shoga yako wa karibu kabisa, ndiye ambaye amekuwa akitembea na mumeo au mpenzi wako. Umekuwa ukimsimulia shida zako na matatizo yako yatokanayo na ndoa yako au uhusiano wenu, yaani mume wako au huyo mpenzi wako kutotulia, ukijua unamsimulia shost wako, wakati ndiye chanzo cha madhila uliyo nayo.

Katika kumsimulia amekuwa akikupa moyo na kukuambia wanaume ndivyo walivyo na wakati mwingine amekuwa akikwambia kwamba, ukiona vipi ni bora uachane naye. Hivi sasa unagundua kwa maumivu kwamba, yeye ndiye ambaye amekuwa akikusababishia maumivu yote. Hebu sema ungefanyaje?
 
Uzuri sina mume wala mashoga wakuwasimulia mazuri na mabaya ya mahusiano yangu...
 
Kwanza ni kosa kumueleza shoga mambo yako yote kama unamueleza basi mpe utandu ukoko uweke mwenyewe manake mashoga wazuri hakuna tena kumebaki mafisadi, nikigundua kama ndio mkwe mwenza nikumshukuru kwa uungwana wake na kufunga njuga kumuweka mumeo atulie ili huyu shostito akijue cheo chake juu yakua inauma sanaaaaaaaaa lakini nikiwa kama mwanamke ntakikisha mume wangu nikonae nimemthibiti....
 
kwangu mie siwezi sema mpaka limetokea lakutokea so far i trust men kuliko hao so called shoga sijui nini kumueleza mambo yangu ........................
 
Usimsimulie mtu mambo yako mwiko, hata ndugu maana watawaambia wengine muyamalize wenyewe. Ukishindwa achana naye
 
Nitahakikisha one night tunashea the same bedi teh teh teh
 
Kinachofuata hapo ngumi tu za mashoga. Kikulacho kinguoni mwako.
 
Hivi kweli mnaweza kukaa kimya au mnadanganya tu humu MMU? Swala la wanawake kuwasimulia mashoga zao juu ya mahusiano yao na wenza wao au wapenzi wao ni jambo ambalo wanawake wengi hufanya sana. Ni wanawake wachache sana wanaweza kuwa hawafanyi hivyo, lakini, hata hivyo kuna baadhi ya siri zao watazivujisha tu kwa mashoga zao aidha kwa bahati mbaya au kwa kukusudia pale wanapohitaji kusifiwa japo kidogo au kuwakoga wenzie kuwa wanacho cha kujivunia................ kuweni wakweli kwa nafsi zenu, msibishe kishabiki.............!
 
Unauliza makofi polisi?

Na mie natembea na mume wangu daima, simpi pumzi tena. Na yule shoga namfunga jiwe la kilo hamsini namtupa baharini

Hebu fikiria kwamba, umebaini kuwa shoga yako wa karibu kabisa, ndiye ambaye amekuwa akitembea na mumeo au mpenzi wako. Umekuwa ukimsimulia shida zako na matatizo yako yatokanayo na ndoa yako au uhusiano wenu, yaani mume wako au huyo mpenzi wako kutotulia, ukijua unamsimulia shost wako, wakati ndiye chanzo cha madhila uliyo nayo.

Katika kumsimulia amekuwa akikupa moyo na kukuambia wanaume ndivyo walivyo na wakati mwingine amekuwa akikwambia kwamba, ukiona vipi ni bora uachane naye. Hivi sasa unagundua kwa maumivu kwamba, yeye ndiye ambaye amekuwa akikusababishia maumivu yote. Hebu sema ungefanyaje?
 
Omba kwenda nao outing wote wawili, huko uwajulishe kama wanachokifanya unakifaham na unaushahid wa kutosha, mtakie rafiki yako kila la kheri apate mume wake na atajua uchungu wa hilo unavokuwa, baada ya hapo kata mawasiliano na huyo rafiki ikiwezekana hama ata nyumba kama ya kupanga ili hasije kutaka kukutembelea na kuomba msamaha, huyo mwanamke jina lake halianzi na M lakini na la baba yake linaanza na M pia, ebu nipm km ni huyo anapenda sana kuchukua waume za rafiki zake ni tabia yake na ameshakorofishana na rafiki zake wengi tu!
 
Back
Top Bottom