VISA NA MIKASA; Shoga ya
Nimetoka zangu kujifungua narudi nyumbani nakuta nyumba ni safi, yaani nawaza huyu si mume wangu kwakweli!
Naingia ndani nawaza nani kafanya huu usafi! Jicho la kiukaguzi, yaani kuchunguza kama kuna kitu. Basi nikawa sina amani, mume ananiuliza vipi namuambia kuchoka tu mume wangu naye anamshangao akiangalia chumba!
Mwanaume akatoka, naanza kukagua nakuta chupi ya kike uvunguni, tena iliyotumika, najua si saizi yangu.
Aisee nilichanganyikiwa. Natoka nnje naingia natafuta namna ya kumuuliza mume wangu nashindwa kitu kimenikaba.
Basi siku hiyo ikapita, nikalala, asubuhi mume kazini, mimi bado nina kisirani, majirani si ndiyo wanakuja sasa.
Kuna jirani mmoja ni kama ndugu, yaani yeye tulikua pika pakua basi akaanza kuniambia.
“Shogaa, nikuambie kitu tu, watoto wako bado wachanga, mumeo atawabemenda, ulipokua huko kila siku anabadilisha wanawake, hata jana kuna Mmama mtu mzima kaja kufanya usafi!”
Nazidi kuchanganyikiwa, naanza kukusanya vitu vyangu kwa hasira niondoke, basi shogaa ananisaidia, ananipampu kukaa mbali na mume wangu.
Tukiwa tunapanga vitu mume wangu anaingia, shoga yangu anatoka harakaharaka.
“Nishakukataza marafiki, huyu umemzoesha vibaya, mambo gani ya kumuambia aje kufanya USAFI, nani alikuambia mimi nashindwa kufanya usafi?
Umesema nimuachie funguo? Unaona kachukua mpaka na vitu vyangu!
Mume anapaniki, nashindwa kuelewa ni nini, namuwakia naanza kumuambia ana wanawake namuambia nimekuta mpaka nguo za ndani!
Hajibu kitu, ananiambia twende, tunafika kwa yule Dada, anamuambia nipe funguo zangu, Dada anang’aang’aa macho, anamuuliza.
“Mke wangu ndiyo alikuambia uingie mpaka chumbani kwangu kufanya usafi?” Nakua sielewi anajitetea.
“Hakuniambia ila niliona kama atarudi kachoka nimsaidie.” Namuonyesha na nguo ya ndani namuuliza yanani anaikana!
“Ilete, si kasema si yake, basi naisagia majivu kizazi kinaoza!” Mume wangu anaondoka anaichukua ile nguo ya ndani na kuondoka nayo mimi na shoga yangu jirani tunashangaa, ila namuona ana wasiwasi sana.
Jioni Dada huyo anakuja, anapiga magoti kuomba nguo yake ya ndani irudishwe, analia, “Sikudhamiria!” Anakiri alitegeshea yeye ili mimi niione kuwa mume wangu alikaua kiingiza wanaume ndani hivyo nikasirike na kuondoka, namuuliza kwanini umeamua kunifanyia hivi, ananaimbai kwakua naringa sana na mume wangu!
Tunamrudishia, anaondoka nimejifunza! Hakuna urafiki wa chumbani! Ingawa sikumuambia mimi kuja kufanya usafi chumbani kwangu lakini ni rafiki yangu ambaye nilishamzoesha mambo mengi, mume wangu alishanikatazaga mambo mengi na yeye lakini sikumsikia ila sasa hivi nimejuta sitaki tena ushoga wakugandana!