DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Shomari Kapombe, beki mashuhuri wa Simba SC, amefanya historia baada ya kupitishwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwenye orodha ya wachezaji 10 bora wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika Ngazi ya Klabu kwa mwaka 2025.
Kapombe ndiye mchezaji pekee kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kuingia kwenye orodha hii, jambo ambalo linatofautisha na wachezaji wengine wote waliotajwa, ambao wanatokea ligi maarufu za Morocco, Misri, na Algeria. Mafanikio haya yanathibitisha kiwango cha juu alichokionyesha Kapombe katika michuano ya kimataifa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la shirikisho barani Afrika, akiwakilisha Simba SC na soka la Tanzania kwa heshima kubwa.
Hii ni hatua kubwa si tu kwa Kapombe bali kwa soka la Tanzania kwa ujumla, ikionyesha kwamba wachezaji kutoka eneo la Kusini mwa Sahara wanaweza kushindana na wale kutoka ligi zenye nguvu barani Afrika. Shomari Kapombe ni beki anayezeeka na utamu wake kwa sasa ana umri wa miaka 33.