Shoppers ya Masaki ni hawana Utu kwa wateja wao

Nadhani shida sio wao shida ni mtandao wako, maana huenda ela ingerudi kwako ushaondoka uwatie hasara.
 
Hata ningekuwa mm ningefanya hivYo wabongo hawaaminiki dk 2 nyingi anakuliza usipokuwa makini next time njoo mwananyamala sokoni.
 
Mambo ya Masaki waachie wenyewe watu wa Masaki, wenzako chupa ya Hennessy wananunuwa kuanzia laki 4, wewe sh 53,000 ambayo anapewa baunsa wa mlangoni kama tip unakuja kutupigia kelele hapa.

Siku nyingine nenda Discount super market ndio wapo kwa ajili ya watu wa Magufuli wanyonge.
 
Tigo wanajua kuwa wanachangamoto katika mifumo yao... Kwa nini wasiset pesa kama imetumwa irudi muda huo huo kwa mtu aliyetuma pesa ili atafute plan B kwa haraka na wepesi zaidi...
 
Sisi zetu ni buguruni sokoni soko la ilala pale nikienda kila kitu kipo na beiii cheee huko kwenye ma supamarket tuwaachie wenye hela.Pole sana ndugu yangu na ww una afu hamsin unaenda kuushtua umasikini supamarket sasa umekutana na fedhehaaaa 🤣🤣🤣
 
Huwa najiuliza, kwanini itumie masaa 72 kurudisha pesa iliyotumia sekunde moja kuichukua?
 
Wabongo mnapenda lawama za kipuuzi sana
 
Hapo huwezi kuwalaumu maana ni biashara sasa pesa hawajapata watakupaje bidhaa?
Tigo wenyewe wameshasema after 72hrs hela inaweza kurudi kwako sasa imagine wao shopppers wangepata vipi pesa yao
Jamani tupunguze kulalamika watanzania
 
Mimi nimeshawahi kuwabadilikia hao wahindi wa mchongo, nikachukua bidhaa, hela ikarudi kwangu ndiyo nikawapelekea, sitakagi ujinga. System malfunction is none of my business, i paid groceries and i want groceries zangu, USIKAE KINYONGE NCHI NI YETU SOTE
 
Hela yenyewe alfu 50 lakini lawama kibaoo.
Kosa ni lako na mtandao wako wa simu lawama kwa mfanyabiashara!!
Siku nyingine njoo ufanye manunuzi Sokoni Temeke Stereo uepuke adha za ushuani.
 
We jamaa si ungeviacha tu kwani ungekufa njaa kwa siku moja?

Masaki ni mahali pa kujiwekea heshima.

Umeonekana umevamia Kambi sio levele yako. Unaona kuacha 51500 ni ishu sana.

Ungeacha vitu kw amakubaliano kwamba ikiwa pesa itakatwa utarudi kuvichukua kwa sababu hapo ni Ofsini. Ila wao hawawezi kukupatia kwa sababu hawajui pakukupata ni wapi.

Common sense is commoni.
 
Hela yenyewe alfu 50 lakini lawama kibaoo.
Kosa ni lako na mtandao wako wa simu lawama kwa mfanyabiashara!!
Siku nyingine njoo ufanye manunuzi Sokoni Temeke Stereo uepuke adha za ushuani.
Watu wanapenda shida......kwanza nenda na cash yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…