Should i attend this wedding

Bado niko kwa hali ya mshtuko kuhusu kifo cha kijana huyu,nilikuwa nimetoka likizo wiki ya kwanza ya January nilipoingia pale kwenye estate ambapo pia mimi ninaishi marehemu na dada huyu tukakutana wakitoka wakaniileza walikuwa wamerudi usiku sana ndivyo sikupata nyumbani nilipo wasili -huyu dada sasa ni jirani yangu.Nilipoenda kusalimu majirani wengine wakanieleza kwamba dada huyu anafanya harusi nikawambia kweli amekaa sana na yule kijana wakanieleza kwamba siyo yeye anamwoa.

Nikastuka sana manake hata fununu ya mtu mwingine sikujua.Huyu kijana akawa analewa sana,amewacha kazi halafu gafla akawa mgonjwa haya yote baada ya kupata habari eti mpenzi wake wa miaka saba anaolewa April.tulikuwa tunafanya kazi na dada yake marehemu so ni watu ninawajua mpaka familia yao.Sasa akalazwa siku mbili tatu maskini akafariki.Kusema kweli ninamulaumu dada huyu kwa kifo cha huyu bwana kwa kumhaada na kumtumia huyu kijana ilhali alijua anamwenza.Bado roho yangu ni nzito sasa tena nimealikwa harusi kabla hata sija process haya ya kifo cha huyu kijana.
 
dah... What a contradiction... How can you love someone and be so mean at the same time...
 
we nenda tu arusini. Karibu kila harusi ina kisa cha namna hiyo japo kiwango cha maumivu hutofautiana. Kufa wanakufa wengi tu, na wengine wanabaki wanaumia bora wangekufa. Tatizo ni kwamba hili limepiga karibu na wewe ukalifahamu kwa undani!
 
duh!! imeandikwa hekima ni bora kuliko maombi!! tumia hekima yako!!!!!!!!!!
 
ayaaaaa.........no....but lazima kuna sababu.......lakini hata wao wanaume si wanatufanyiaga hivyo hivyo bana......mpaka tunajitoa uhai....kwa hiyo si mbaya sana we nenda kale mikuku huko kwa raha zako

Haataa wewe? Temea mate chini.
 
Nakushauri usiende kuonyesha hujapendezwa na jambo alilolifanya huyo dada. Haimaanishi unamhukumu, bali unaonyesha hisia za kibinadamu za kutokubaliana na uovu.
 
Kama roho yako inakuwa ngumu usiende maana usije ukawa na sura ya msibani ukaharibu picha za harusi ya watu bure
 
Ulisha kula mnuso wa msiba, achana na huo wa harusi. Hukumu iskupitie bure.
 
Nenda kwenye harusi....hayo mengine mwachie Mungu....after all hujui mengi sana na pengine unachofikiri kuwa chanzo cha kifo sicho...binadamu wana siri nyingi sana.....!!!
 
Haataa wewe? Temea mate chini.

siwezi temea mate chini coz hata sisi wengine yalishatukuta bahati mbaya hatukufa......tunamshukuru muumba kwa kutuumba na shoku abzoba za roho aina ya rob magic
 
Jamani wengi tunamlaumu huyo dada lakini kama legends wanavyosema 'every story has two sides' sasa kama huyo kaka (rip) alikuwa hana nia ya kumuoa huyo dada mlitaka afanye nini? Maana sio kila mwanaume ana mipango ya kuoa.

Wewe kama nafsi unakusuta usiende, ila mweleze sababu at least you owe her that.
 
siwezi temea mate chini coz hata sisi wengine yalishatukuta bahati mbaya hatukufa......tunamshukuru muumba kwa kutuumba na shoku abzoba za roho aina ya rob magic

Ubarikiwe kwa kuwa mkweli.... nakutumia popcorn kama za jana....:wink2:

The Following User Says Thank You to Preta For This Useful Post:

Michelle (Today)​
 
Mh balaa,, vicheche everywhere,,,,
 
Ulisha kula mnuso wa msiba, achana na huo wa harusi. Hukumu iskupitie bure.

hihihihihihi......hebu geuza upande wa pili je kama huyo kaka alikuwa ndio anaoa na dada akakufa halafu wewe ndio rafiki wa kaka......ungeenda harusini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…