Ati huwezi kulinganisha England na Tanzania. Hivi kitu kizuri kikifanywa na adui yako au rafiki huwezi kukiiga? hapo ndio tunapopotea kuendekeza kichwa ngumu ya kiuendawazimu - we do this in Tanzania, ..........
Croatia wangekuwa wanaweweseka kama baadhi ya members wa JF wasingeweza kuwafunga England walipocheza nao pale Wembly Stadium kwa sababu wakisikia jina tu ni jinamizi tayari. (Wanja la kimataifa historia ya soka na madoido kibao). Wenzetu hawaweweseki na jina wanacheza mpira waliofunzwa.
Kocha wa Croatia analipwa karibu £ 20,000 kwa mwaka wakati mwenzake wa England anapata takriban £ 3,000,000. Matokeo mmeyaona.
Msingi wa swala langu: Kwa sababu hata mshahara wa Maximo ni mkubwa kupindukia na usiri ulio katika mkataba wake tumeingizwa kwenye mkenge, ni bora hizo pesa wangelipwa makocha angalau 20 na ushee wafundishe mpira kuanzia shule za chekechea, primary na secondari na kuongeza vipaji ambavyo tayari vipo Tanzania. Maximo ni mbabaishaji mwingine tu ambaye anaona achume kwa vilaza ambao wamempa ulaji.
Huyu ameshindwa mbinu ndogo tu ya kuwafunga Mozambique timu ambayo tuliweza kutoka nayo sare nyumbani kwao, ilibidi abebe lawama zote na kufukuzwa. Sasa hao Mozambique wana quality gani ya ajabu ya kutubugiza magoli au kutoka nao sare?
Ukiboronga na kuleta uvundo ni sharti uache mwenyewe kwa hiari yako au ufukuzwe ndio mfano ambao tunatakiwa tujifunze kutoka kwa wenzetu wa England. Tofauti na sisi Tanzania ukivurunda unahamishwa kwenda sehemu nyingine ili uendeleze libeneke la kuboronga au wanakubakiza pale pale, na hili sio geni wala sio kwenye michezo tu kwenye nyanja mbali mbali hakuna uwajibikaji, madudu ni yale yale waziri anasaini mkataba halafu anasema sheria zetu ndio zenye tatizo wakati yeye amepewa dhamana kuangalia maslahi ya taifa. Wewe ni waziri kwa nini uweke sahihi wakati sheria ina walakini? Badili sheria then saini mkataba ndiyo kazi hiyo hawakukupa uwaziri bure wala sio mbumbumbu unatakiwa uwe na telescopic eyes kuona dosari kama sheria mbovu omba Bunge waibadili mara moja.
Angalia timu kama Arsenal wana wachezaji wengi ambao sio Englanders sasa huko walikotoka nani aliwafundisha? Unapoongelea diet unaniacha hoi unafikiri packed lunch ndiyo zinasaidia ushindi? Usizugike na neno proffessional tulikuwa na wachezaji wengi ambao waliendeleza vipaji vyao tangu wakiwa wadogo nitakupa mfano wakati tulikwenda fainali Nigeria tulikuwa na kina Peter Tino ambaye alifunga bao la kutupeleka kwenye fainali tena ugenini Zambia, alikuwepo Mohamed Salim huyu baadae alinunuliwa uarabuni, walikuwepo wachezaji wengi wazuri akina Manara, Pondamali, T. Ally n.k. na tuliweza kufanya vizuri. Kwenye riadha ndio usisema walikuwepo akina F. Bayi, Nyambui, n.k. Hivi ni vipaji vilivyojengwa tangu wakiwa wadogo sio kuleta uchuro wa kupoteza pesa za walipa kodi kwa siri siri. Hatuhitaji hizo diet pumba ili tuwe na ushindi, badget constraints wakati walikaa Brazil mwezi mzima? Tena wakaenda Scandinaviana countries naona hata data ndogo tu huna.
Kumbuka wakati timu ya kenya walipotufunga magoli matatu mtungi kule Nairobi wakati wachezaji wetu mashuhuri hawakwenda kwenye mechi ile na nini kiliwapata walipotua Dar? tuliwanywesha magoli matano mtungi. Hatumuhitaji huyu mbabaishaji kutoka Brazil.
Ati huwezi kulinganisha England na Tanzania. Hivi kitu kizuri kikifanywa na adui yako au rafiki huwezi kukiiga? hapo ndio tunapopotea kuendekeza kichwa ngumu ya kiuendawazimu - we do this in Tanzania, ..........
Tanzania katika soka inaweza kuwa kama England siku moja lakini kwa hivi sasa hiyo siku haipo karibu,it will take time. Maximo anahitaji muda, kumfukuza au akijiuzulu sasa hivi tutaajiri kocha mwingine ambaye nae ataanza mwanzo tena, it will be a step back, we need to be patient.
Hivi wewe Dua unafuatilia masuala ya mpira kweli? na siimanishi soka la bongo tu, naamisha world soccer.Blah blah hapa ni nyingi, au na wewe ni mmojawapo wa wale watu wanaokusanyika nje ya klabu za yanga na simba na kujadili habari za magazeti ya kidaku?
Croatia wangekuwa wanaweweseka kama baadhi ya members wa JF wasingeweza kuwafunga England walipocheza nao pale Wembly Stadium kwa sababu wakisikia jina tu ni jinamizi tayari. (Wanja la kimataifa historia ya soka na madoido kibao). Wenzetu hawaweweseki na jina wanacheza mpira waliofunzwa.
Lets get back to business- Croatia unavyoiongelea hapo juu unaonekana huwajui kabisa, unawaongelea kama katimu kadogo kasikojua mpira. Let me educate you a little bit kuhusu hawa mabwana. According to current FIFA Ranking- Croatia ni bora kuliko England, wako kwenye top 10 ya dunia ambayo inaongozwa na Argentina kwa sasa.Kwa hiyo jina la Croatia ni kubwa kuliko England kwenye international football scene na wala hawakuwa na sababu ya kuweweseka kwa kuwa waliingia wembley wakiwa top of their group na wameshaqualify.
Kocha wa Croatia analipwa karibu £ 20,000 kwa mwaka wakati mwenzake wa England anapata takriban £ 3,000,000. Matokeo mmeyaona.
Kwa mshahara huo wa Coach wa England,ukiboronga ni lazima uachie ngazi- its plain simple. Utaona kwamba hata kama Croatia ingefungwa kelele zisingekua nyingi toka kwa mashabiki wao coz they know they fall short in resources.
[B]Msingi wa swala langu: Kwa sababu hata mshahara wa Maximo ni mkubwa kupindukia na usiri ulio katika mkataba wake tumeingizwa kwenye mkenge, ni bora hizo pesa wangelipwa makocha angalau 20 na ushee wafundishe mpira kuanzia shule za chekechea, primary na secondari na kuongeza vipaji ambavyo tayari vipo Tanzania. Maximo ni mbabaishaji mwingine tu ambaye anaona achume kwa vilaza ambao wamempa ulaji.[/B]
Mtu yeyote anaefuatilia mpira kwa karibu hawezi kumuita Maximo 'mbabaishaji' au una personal issue naye mazee? Ngoja nikupe few lines nilizozidonoa kwenye CV yake.... 92/93 Brazilian National U-17, U-20 and Olympic Teams.(Kabla sijaendelea- unamjua Ronaldinho? naye alikwepo kwenye hao vijana aliowafundisha) baada ya hapo- 1993-94 First Team-Assistant Coach for Qatar National Team, Head Coach and Supervisor of the training centre of Rio De Janeiro for IFC Union Berlin in 1998, akaenda Scotland kama head coach wa Livingston FC in 2003/04. On top of that jamaa amepiga shule- ana graduate and post-graduate degrees ya Technical and Physical Education, Tactical and Technical Football na Sport Training Methodology ya University of Federal of Rio de Janeiro. Surely, there must be some few other better words to descibe him rather than 'mbabaishaji'. Unasema '..ni bora hizo hela wangelipwa makocha 20..', ni wazi kuwa wewe unajali wingi badala ya ubora. Na huko chekechea na mashuleni unaposuggest makocha waajiriwe-ni lazima ujue kwamba kuna watoto wengi wenye vipaji vya michezo tofauti, sasa kwa nini mpira tu ndio upewe kipau mbele hadi makocha wachukue ajira za walimu? I understand kuwa serekali imekubali kuajiri jamaa wanye degree za PE kwenye mashule, hawa ni maspecilist kwenye michezo yote,this is a step forward lakini pia subira inahitajika kwani matunda yake yanaweza anza kuonekana in 10 years.
Huyu ameshindwa mbinu ndogo tu ya kuwafunga Mozambique timu ambayo tuliweza kutoka nayo sare nyumbani kwao, ilibidi abebe lawama zote na kufukuzwa. Sasa hao Mozambique wana quality gani ya ajabu ya kutubugiza magoli au kutoka nao sare?
Mozambique wana quality gani? Again, nakurudisha kwenye FIFA ranking, Black Mambas wapo nafasi ya 75 na Tanzania ni ya 105, ranking ya CAF inawaweka Msumbiji kwenye nafasi ya 15 wakati TZ ni ya 26. Kwa mantiki hii ni kwamba mpira wa hawa chingas ni better than South Africa, Trinard and Tobago and Jamaica just to mention some few big names ambazo zimewahi kushiriki World Cup recently na zina wachezaji kwenye ligi kubwa za ulaya. Je unajua kuna wamachinga wanachezea Benfica na Sporting Lisbon? Wakati sisi tumeshiriki kwenye African Cup of Nations mara moja tu, wenzetu wao ni mara tatu. Kuna factors nyingine pia ambazo ni psychological, hawa wenzetu wana insipirational figures, watu ambao wametesa na bado wanaendelea kutesa kwenye ulimwengu wa soka la kimataifa., talk about Eusebio, Carlos Quiroz, Abel Xavier- hawa wote ni machinga and every young boy who is playing footbal in that country today is dreaming of being like them one day.Sisi tunao kina nani? Peter Tino?(Naskia karibu gongo litammaliza, mabega yamesha overtake kichwa!) Pondamali? Manara? Did they ever play for Liverpool, Benfica or Sporting? Wana mafanikio gani kutokana na mpira wao ili wadogo zetu watake kuwa kama wao? No wonder wazazi wanawahimiza watoto wao wakazanie masomo na sio kucheza.
Ukiboronga na kuleta uvundo ni sharti uache mwenyewe kwa hiari yako au ufukuzwe ndio mfano ambao tunatakiwa tujifunze kutoka kwa wenzetu wa England. Tofauti na sisi Tanzania ukivurunda unahamishwa kwenda sehemu nyingine ili uendeleze libeneke la kuboronga au wanakubakiza pale pale, na hili sio geni wala sio kwenye michezo tu kwenye nyanja mbali mbali hakuna uwajibikaji, madudu ni yale yale waziri anasaini mkataba halafu anasema sheria zetu ndio zenye tatizo wakati yeye amepewa dhamana kuangalia maslahi ya taifa. Wewe ni waziri kwa nini uweke sahihi wakati sheria ina walakini? Badili sheria then saini mkataba ndiyo kazi hiyo hawakukupa uwaziri bure wala sio mbumbumbu unatakiwa uwe na telescopic eyes kuona dosari kama sheria mbovu omba Bunge waibadili mara moja.
Maximo sasa hivi ni kama mhudumu wa hoteli ambaye anakipresent chakula mezani na kukutana na jazba za wateja kama wewe lakini watu wanasahau kwamba yeye sio mpishi wa chakula hicho, tumpe nafasi akipike chakula chake mwenyewe.
Angalia timu kama Arsenal wana wachezaji wengi ambao sio Englanders sasa huko walikotoka nani aliwafundisha? Unapoongelea diet unaniacha hoi unafikiri packed lunch ndiyo zinasaidia ushindi? Usizugike na neno proffessional tulikuwa na wachezaji wengi ambao waliendeleza vipaji vyao tangu wakiwa wadogo nitakupa mfano wakati tulikwenda fainali Nigeria tulikuwa na kina Peter Tino ambaye alifunga bao la kutupeleka kwenye fainali tena ugenini Zambia, alikuwepo Mohamed Salim huyu baadae alinunuliwa uarabuni, walikuwepo wachezaji wengi wazuri akina Manara, Pondamali, T. Ally n.k. na tuliweza kufanya vizuri. Kwenye riadha ndio usisema walikuwepo akina F. Bayi, Nyambui, n.k. Hivi ni vipaji vilivyojengwa tangu wakiwa wadogo sio kuleta uchuro wa kupoteza pesa za walipa kodi kwa siri siri. Hatuhitaji hizo diet pumba ili tuwe na ushindi, badget constraints wakati walikaa Brazil mwezi mzima? Tena wakaenda Scandinaviana countries naona hata data ndogo tu huna.
Yaani hujui kwamba vyakula na vinywaji wanavyokula wachezaji vina effects kwenye performance yao? Yaani hujiu kwamba kila proper football club au professional footballers wana dietitians? Kwa taarifa tu ni kwamba current Arsenal squad imejengwa na vijana wengi waliosajiliwa wakiwa watoto wadogo, some of them went there when they were 14! Walikua spotted na mascouts wa club ambao wako all over the world, walibahatika kukutana na watu walioona vipaji vyao na wakapelekwa hapo kuendelezwa.Waliosajiliwa wakiwa wameshaiva kama Lehman,Rosicky, Hleb, Sagna wametoka kwenye vilabu vingine ambavyo pia vipi kwenye top leagues za dunia hii. By the way.... hakuna mtanzania anaechezea Arsenal!
Unaonekana unabisha kwamba suala la budget constraint halipo kwenye TFA, umesahau kuwa kuna kampuni moja ya Bia ndio ilidhamini hizo safari huko majuu? Pamoja na hayo bado ni kichekesho kufananisha hela waliyonayo TFA na FA. Kama ingetokea timu za Tanzania na England zikawa huko scandinavia-ie Sweden kwa wakati mmoja- scenarios zingekua hivi: England watakaa kwenye one of the top 5 stars hotel wakati Stars watalala kwenye cheap B&B (tena wanaweza wakashare rooms!).Ukija kwenye msosi ni basi tu hakuna mama ntilie ulaya lakini wangekwepo vijana wetu wangepelekwa huko wakati wenzao wa England wakijidai na buffet!Viongozi wa timu wanapiga panga umoumo.
So timu yetu ya Taifa iliua majuu kwa mwezi mzima! ndio uone tofauti iliyopo kati yetu na timu ya Taifa ya england, they dont need kukaa kambini mwezi mzima- hata kama wanajiaandaa na kombe la dunia, ndio maana nasema inachukua muda mrefu sana kuwaandaa wachezaji wetu tofauti na wenzetu ambao mambo mengi wanayafanya kwenye club zao wakikutana ni technical issues kwa sana na sio kukimbizana na kupigishana push ups.
There is no doubt anyone deserves a sack kama ni kocha wa England na umeshindwa ku qualify for EURO 2008 lakini its so unfair for anyone to start calling for Maximo's head, common Dua-be serious.