Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Watu kama ninyi mnachangia sana hizi statusquo ziendelee...Mungu amekuumba wewe sawa na hao unaowaita wazito, you start failing the moment you see wengine ni wazito na wewe ni mwepesi...

I have, am will continue to chanhe things for the benefits of all...Si amini katika binadamu kuamua hatima yangu, isipokuwa Mungu.
 
Kabla ya kwenda huko kwenye uzoefu, tuone uzoefu huo unapatikanaje kama si watu kuchomekwa chomekwa ili kutengenezewa CVs. Kuna watu wakifungua tu midomo kuongea unagundua hekima yao, incompetence ndiyo inayoanza kuji display kinyume na hadhi za majina ya nafasi walizonazo.

Wapendwa haidanganyi, bila competence no solutions to existing problems, sanasana tusipoangalia ipo siku tutachapana ili kuondoa hii statusquo...changes are there to stay ni kanuni ya nature, ila yasipokuwa programmed huja kama mafuriko na kuharibu badala ya kujenga
 
Kuteua mtu kwenye senior positions tena kutoka nje ya Serikali bila kufuata seniority naona kuna shida hapa,wengi wao wameshindwa kuongoza taasisi kilichobaki ni kuwa machawa ili kuficha mapungufu yao.
Nashauri Serikali ifuate utaratibu iliyouweka yenyewe sio mambo ya kujuana.
 
Exactly...Tume set precedence mbaya sana...Na ukiangalia hii imesababisha hao wateuzi kuchagua weak beings ili wafiche incompetence zao...The cost goes to the entire society, mbaya zaidi mambo hayo yameenda mpaka kwenye universities kitu ambacho kitaua hata innovation na mentorship ambayo ndiyo key kwenye carrier growth hasa hasa za militia na academics...

Cry my country, kila mtu kageuka kuwa chawa wa yule anayedhani anamanufaa zaidi kwake na familia yake...Hakuna tena kujali maendeleo ya nchi na watu
 
Nadhani taasisi zimshauri mama inavyotakiwa waache mifumo ifanye kaI sio mtu kuifanyisha kazi mifumo
 
Security of tenure kwa mawaziri ambao wata fail ni kosa
Imagine Dorothy angekuwa nayo wizara ya afya
Pascal Mayalla
Kwa sasa mawaziri ni wanasiasa na sio profesionals, hiyo Security of tenure ni kwa top brains, watu waombe kazi, washindanishwe, ulioana jinsi CJ wa Kenya alivyopatikana?.
P
 
Sijasoma contents. Lakini heading inatosha kusema you are right.


Kuna watz wengi wenye ujuzi kuzidi hata hao wabunge.
 
Leo DGIS nae pia ametumbuliwa kimya kimya bila maelezo yoyote!.
Kiukweli kumtoa mtu kwenye position ya DGIS na kumwacha popote nchini is a mistake!. Position stahiki kwa DGIS mtumbuliwa ni kumpeleka ubalozini. Rais nae ni binadamu na sio malaika, hivyo anaruhusiwa kufanya human mistakes. Hili nililizungumza hapa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Kuhusu hizi appointments nyeti na very strategic tusimwachie mtu mmoja tuu, she is human hivyo sometimes human mistakes caused by human weaknesses zinaweza kutokea ukajikuta unamtumbua mtu mzuri kwa issues ndogo tuu zikingine za ... Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
 
Akimpeleka ubalozini atashindwa KU mmonitor vizuri!!

JAPO kwa sura makini kama ile!ILI deserve More,sio kuwa monitored in corridors!

Mungu IBARIKI NCHI yetu TANZANIA tuipendayo!
 
Washauri wanaomzunguka ndo tatz, maamuzi makubwa kiasi hicho hafanyi bila kushauriwa.

Kama ni wengi wapunguzwe.
 
Teuzi nyingi zinafanywa kwa kujuana na mapendekezo ya Chawa wa mama.Huyu ni Mwenzetu au wazazi wake walikuwa wanachama na viongozi wa mwanzo wa Tanganyika huru au baraza la Mapinduzi Zanzibar.Kwa hiyo hata wakiharibu,wanakingiwa kifua,na wazee wao
 
Mimi nadhani awe anatoa pia na sababu ya kuwatengua hao wateule wake, ili na sisi wananchi tuwe upande wake katika hayo maamuzi yake.
Naunga mkono hoja, kiukweli katiba yetu, sheria zetu, taratibu zetu na kanuni zetu, zinamapungufu makubwa!.

Kwenye presidential appointments powers, rais anaweza kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, bila kutoa sababu yoyote ya appointment hiyo kwa yeyote, na pia anaweza kutengua uteuzi wowote kwa yeyote bila kutakiwa kutoa sababu zozote!.

Mtu akiishateuliwa na rais kwenye public office, huyu sasa ni mtumishi wa watu, japo ni msaidizi wa rais, lakini sio mtumishi wa rais!. Watumishi wa rais ni wale wanaomtumikia yeye ofisini kwake, nyumbani kwake na dereva wake, kama hawapendi anawaondoa tuu bila kutoa sababu yoyote.

Lakini kwa public servants waotumikia public, wakitenguliwa, the public has the right to information kwanini wametenguliwa!.

Baada ya kumtengua Balozi Mulamula, kukatokea vineno... hivyo nikashauri Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Kwa jinsi ninavyomfahamu huyu jamaa Sijui kafanya nini kustahili kutimuliwa!, ila kwa maoni yangu, huyu jamaa ni mmoja ya majitu very bold pale Wizarani, ambao serikali yetu imebahatika kuwa nao, hili jamaa limesimama wima kusimamia ukweli no matter what!, na kiukweli tulifanikiwa sana kudhibiti makuwadi wa mafuta na kuzuia ma cartels!. Wakati wa upungufu wa mafuta ya petrol, nilifanya nae mahojiano marefu
View: https://youtu.be/s-ZYP33jjww?si=FQJucdhOK-p1gxPh . Kiukweli the guy is smart!, sijui kumetokea nini?!, ila ukiwa mkweli mno, katika corrupt system, sometimes unaonekana kikwazo!. Issues kama hizi ndizo za sisi waandishi makini kuzifanyia IJ.

Tanzania tunajikuta tunapoteza watu wazuri, wachapakazi, waadilifu kwa majungu tuu na fitna ndio maana tunasisitiza, kwenye kuteua, kwasababu kuna sifa na vigezo, sio lazima tuambiwe sababu za fulani kuteuliwa, hata akiwa ni mkwe wa rais, ndugu, jamaa au marafiki, ni sawa tuu alimradi anakidhi vigezo, lakini kwenye kutumbua, lazima tuwe tunaelezwa sababu not necessarily in details.

Japo kuna kitu kinaitwa the right to privacy, but when it comes to public offices and public offices there is no right to privacy besides yale ya nyumbani!, whoever paid by taxpayers money, the taxpayers have the right to information public and private conduct of their leaders because it's there money!.
P
 
Wazo la transparency ni zuri ila hakuna muimili uko huru.
 
Ili ni Jambo ambalo nimelifikiria Sana miezi ya ivi karibuni ,

Waziri alipaswa achaguliwe kiuwezo Zaid yaan awe amefanikiwa kila Kona kielimu,kiuchumi,na awe ameshakuwa kiongozi katika taasisi flani na zikafanikiwa,

Mfumo huo huo utumike kwa wakuu wa mikoa,wilaya na secta mbali mbali

Mbona private mkurugenzi lazima uwe reputation nzur na lazma ulete matokeo ukishindwa anatafutwa mwingine atakaye kuwa na matokeo kuliko wewe
 
Tanzania tunajikuta tunapoteza watu wazuri, wachapakazi, waadilifu kwa majungu tuu na fitna
1000% tena ndio™ yetu ya hivi karibuni.
Lakini kwa public servants waotumikia public, wakitenguliwa, the public has the right to information kwanini wametenguliwa!.
...wapo wajinga na mafirauni waliodai na wanaendelea kudai kuwa, kutenguliwa kwa public servant ni ukatili wa hali ya juu-hata kama waliokumbwa ni mafisadi, masaliti n.k n.k haswa kama tunambiwa sababu za kutenguliwa ni e.g Ulevi kazini, uhaini na kutoheshimu madaraka and so on. Na kwa hayo pamoja na mengine mengi, ndio naona tulivyojaliwa na majungu.

Anyways sitaenda mbali, right to information or not, nadhani kwa huu utamaduni tunaoigiza kutoka huko majuu, tunachangnyikiwa kiasi kwamba hatujui hata na la kufanyia information hiyo ikitolewa.

R.I.P Magufuli Mtumbuaji wa Haki....Leo nimekukumbuka.
 
Majungu na fitina ndani ya CCM ni kama Uji na Mgonjwa !!
Na Taifa limekubali kuimba hiyo Chorus inayotoka Chamani !!
Fitina majungu na kashfa za kuchongwa ndio habari ya mjini !
Baadhi ya watu wanapata Kula yao kwa kazi hiyo !!
Na kuhusu Katiba wala haihitaji kuzunguka sana kuelezea mapungufu yake kwa maana hata Mwalimu Nyerere ambaye aliisimamia hii Katiba kuandikwa kama ilivyo , baadaye aliiogopa na akatuonya kwamba itatuletea shida kubwa na moja ya shida hizo ni Udikiteta !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…