Naam shuqraani
Natamani kumjua mwandishi wake
Hicho kitabu nilichonacho ni edition ya mwaka 1993, kitabu original kipo katika kiingereza na kilitungwa na Shakil Ahmed Munir mwaka 1978 huko Nigeria, chini ya ; Ahmadiyya Muslim Mission, 45, Idumagbo Avenue, S.L.P 418, Lagos, Nigeria.
Chapa ya kwanza ya tafsiri yake kwa kiswahili imetoka mwaka 1980 huko kenya Chini ya jumuiya ya Waislamu waahmadiyya, S.L.P 40554, Nairobi, Kenya.
Hii edition niliyonayo ni ya mwaka 1993 imetolewa na Jumuiyya ya Waisilamu wa Ahmadiyya S.L.P 376 Dar es salaam, Tanzania.
Katika kitabu hiki Sijaonaa anuani zaidi ya hizo nilizoweka hapo juu, nadhani kwa mawasiliano ya jinsi ya kukipata hapa Tanzania unaweza kuwasiliana na Jumuiya ya Ahmadiyya popote pale ambapo kuna tawi la jumuiyya hiyo hapa nchini au unaweza kutafuta E mail adress ya makao makuu ya jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania ili kuulizia kitabu hicho.
Binafsi yangu nimeona ni kitabu kizuri sana kimeelezea kwa kina juu ya hiyo sanda ya Yesu (Shroud of Turin) na kwa vipi inahusushwa na Yesu na kwa ushahidi uliowazi wa vituo vya kimataifa vya uchunguzi vilivyopewa ruhusa na kanisa katoliki kuifanyia uchunguzi hiyo sanda.
Pia kinaeleza habari iliyofichikana/iliyofichwa juu ya Safari ya Yesu baada ya tukio la msalaba [NI HABARI YA KUSHANGAZA SANA ILIYOJAA USHAHIDI MTUPU].
Jambo lingine kubwa lililofichikana/lililofichwa ni maisha ya Yesu katika nchi nyingine ya mbali baada ya tukio la msalaba hadi alipofariki huko katika hiyo nchi na kaburi lake lipo katika hiyo nchi hadi leo hii, umewekwa ushahidi wa kihistoria, kifupi ni kwamba Yesu hakupaa mbinguni kama inavyoaminiwa kimakosa na watu wengi duniani.
Nimekudonolea kidogo tu ni bora tafuta kitabu hicho usome wewe mwenyewe.