Shtuka, WhatsApp inaweza kuwa 'Surveillance tool' unayotembea nayo

Shtuka, WhatsApp inaweza kuwa 'Surveillance tool' unayotembea nayo

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
346
Reaction score
2,968
Kuna mambo kadhaa katika activities za WhatsApp yanayoweza kufuatiliwa (tracked) hata kama kuna usimbaji fiche wa mwisho-hadi-mwisho (end-to-end encryption), hasa kupitia ukusanyaji wa data-mama (metadata) (kama vile ni nani uliyewasiliana naye, lini, na anwani yako ya IP), udhaifu wa kifaa kupitia programu za ujasusi (Spyware), udukuzi wa akaunti, au backups za chats ambazo sio encrypted.

Ingawa maudhui ya chats yanaweza kuwa ya faragha, taarifa kuhusu unaowasiliana nao na mienendo ya matumizi bado hukusanywa na WhatsApp/Meta na zinaweza kupatikana na Vyombo vya Sheria kwa maombi ya kisheria au kupitia njia zisizo sahihi (malicious attempts) ikiwa kifaa kitadukuliwa (kuwa compromised). Ukiangalia, watu wengi hamfanyi updates za apps na wengine hata Operating System (OS) ya simu zenu.

Mambo gani yanaweza kuwa tracked unapotumia WhatsApp:
  • Ukusanyaji wa Metadata: WhatsApp (na kampuni yao tanzu, Meta) hukusanya metadata, ambazo ni details kama namba za simu za watu uliowasiliana nao, muda gani na mara ngapi unatumia app yao, huchukua IP yako, pia na patterns za namna unavyowasiliana. Taarifa hizi zinaweza kutakiwa na vyombo vya usalama katika nchi kadhaa.
  • Udhaifu wa kifaa chako (Device Vulnerabilities): Endapo simu yako imekuwa infected na spyware au malware, washambuliaji wanaweza kufuatilia chats zako za WhatsApp moja kwa moja, bila hata Meta kujua. Hakuna cha Encryption.
  • Uingiliwaji wa Akaunti (Account Hacking): Unaweza kufanyiwa "Unauthorized access" kwenye simu yako na akaunti ya WhatsApp (e.g., mfano kuibiwa verification code) ambayo hupelekea mtu wa pili kuingilia chats zako. Mnaotumia WhatsApp Desktop baadhi huenda mshakumbana na hili.
  • Cloud Backups: Kufanya backup katika cloud services kama iCloud or Google Cloud kunaweza kusiwe encrypted by default, ambayo inatengeneza tobo la kuwa hatarini. Na wengi hufanya hivi.
  • Linked Devices: Unaweza kupata alert kuwa WhatsApp account iko linked na another device bila wewe kufanya hivyo. Daima angalia "Linked Devices" setting kwenye app ili kuhakikisha hakuna kifaa kingine kinatumia WhatsApp yako.
 
Hakuna Siri mkuu ,Wala hakuna kinachofichika .mimi naamin google ndio kitu hatari zaid,wanajua ni nin unalendelea ni wapi ulipo .
Pia baadhi ya simu sio salama sana ,kama ukienda kinyume na maslahi ya wakulungwa ndio utagundua hujui
 
Sawa, tuambie tuambie.. Tuanye nini sasa.
Apps zinazokueleza wazi juu ya sera yao ya faragha ni za kuzingatia.

Sehemu ambayo hufuatiliwi namba ya simu wala location, ni sehemu muhimu.

Telegram, Signal, Threema ni alternatives nzuri sana za WhatsApp linapokuja suala la faragha.

Humu JF, ni sehemu mbadala pia
 
Back
Top Bottom