LGE2024 Shughuli za uandikishaji haziwezi kuwa na amsha amsha katika mazingira ambayo inajulikana nani atashinda!

LGE2024 Shughuli za uandikishaji haziwezi kuwa na amsha amsha katika mazingira ambayo inajulikana nani atashinda!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Tuwe wakweli na serikali pamoja na wadau wengine tutoke kwenye blanketi la unafiki inajulikana wazi kwamba mahali popote ambapo matokeo ya uchaguzi yanatabirika, hakunaga ari ya ushindani.

Watu huona kwamba hakuna sababu ya kwenda kupangishwa foleni na kupigishwa kura wakati hata mshindi mwenyewe anajulikana.

Ombi langu kwa serikali hebu irekebishe Sheria ili kuruhusu uwanja mpana wa ushindani Sheria kama vile kuruhusu mgombea binafsi na kurekebisha muundo wa tume ya uchaguzi.

Soma Pia: Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Naona kabisa tunaharibu rasilimali nyingi za nchi kuhamasisha watu kushiriki shughuli za uchaguzi likini watu hawaoni sababu.
 
Neno yanatabirika ni kupotosha au kuremba maneno.Ungeandika wizi wa kura na kutangazwa washindi wale walioshindwa imekuwa tatizo kubwa.Refer maneno ya Nape.
 
CCM ndio imetufikisha hapa na hatujui tutatokajee Kwenye huu mfumo wao maana c poaa
 
Serikali ijitafakari sana sanaaa haya tunayoyaona sio picha nzuri kabisaaa kwa kifupi watu WAMESUSIA kabisaa ukipita kwenye vituo unakuta watu wanne watano tu ukipita tena unamkuta karani anapiza zogo na mkewe kwenye simu badala ya wao kujitafakari wamekosea wapi eti wanaenda kusomba wanafunzi mashuleni sijui nani anashauri mambo haya sijui kwa kweli
 
Back
Top Bottom