Shughuli za uokoaji zinaendelea kuwaokoa watu 22 waliofukiwa kwenye mgodi wa madini Tanzania

Shughuli za uokoaji zinaendelea kuwaokoa watu 22 waliofukiwa kwenye mgodi wa madini Tanzania

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Huduma za uokoaji zinaendelea kuwaokoa takribani watu 22 waliofukiwa na kifusi, katika machimbo ya dhahabu ya Nyandolwa, Shinyanga Tanzania.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema tukio hilo limetokea wakati mafundi wakiufanyia ukarabati mgodi huo na kwamba mpaka jana usiku watu watatu walikuwa wameokolewa.

Mboni Mhita amesema wanachokifanya sasa ni kutengeneza njia ambayo ni salama zaidi kuweza kuwafikia.

‘’Changamoto iliyopo ni kwamba eneo lina mawe sana sio eneo ambalo ni teketeke. Ni toauti na maeneo ya uchimbaji ambayo ni teketeke’’, amesema.

Ametoa wito wa ukarabati wa mashimo ya machimbo ya madini kabla ya shughuli za uzalishaji kuanza.

Matukio ya wachimba madini kunaswa katika machimbo si mageni nchini Tanzania kwasababu ya vifaa duni vya uchimbaji wanavyovitumia.
 
Back
Top Bottom