Kwa swala la ajira inaonekana pana uendawazimu serikalini. Hakuna mipango madhubuti ya idara gani inahitaji wafanyakazi wangapi na kuanzia lini. Nadhani kulalamika si swala la msingi japo watu wamewekeza pesa zao ili kuwezeshwa baasaye kwa kupatiwa ajira. Watu watambue kuwa umefika wakati kubuni vitega uchumi mbadala kupata mafao pasi itegemea JKism na Mulogosm. Kwa kuwa na vitega uchumi na kushughulika ipasavyo, tutajikuta hatuteteleki na kauli zao zisizo na lesson plan na hivyo watapo amua kuajiri hakuna mwenye haraka na kupaparukia ajira wakati tayari anapahala pa kushika. Toka watu wamalize vyuo mei/Juni 2012 ni karibu miezi saba. Tutafakari, tungekuwa tumewekeza katika vitegauchumi mbalimbali kwa muda wote huo tungekuwa wapi? na nani angalilia ajira asaivi? Wanayasikia sana malalaniko ya watu ila ndo yanawajaza viburi na kusema wacha hawa vibuyu wasugue benchi. Hii iwe somo kwa wahitimu wa mwaka huu japo wao itakuwa next to the "general election" yaweza kuwa nafuu.Nasisitiza kujishughulisha maana tutambue kuwa baada ya msoto kitaa sasa utakuja msoto kituoni pa kazi. Watazungusha malipo hadi mtu uinunie kazi na kubomoa nchi badala ya kujenga. Sina hakika kama kutotoa majina nakuajiri watu mapena kunaendana na kuwepo ama kutafutwa pesa ya kuwalipa pindi tu walipotipo vituoni kwao. Jamani Mimi simo na wewe haumo ila sote twahusika si tu kwa ajira za waalimu bali idara zote ziitajizo waajiliwa!!