Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Hio usiku unakula chakula gani?au chochote kile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri wako [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabadiliko yanaanza na wewe. Mimi nimeweza kubaki na kg 72 kwa muda zaidi ya miaka 15. Siri kubwa ni mazoezi na kutokula hovyo. Mimi sio mlaji naweza hata kusahau kula.

Nikiongezeka sana 74kg, nikipungua sana 70kg. Kikawaida nakuwa na 72kg

Duuh hongera sana aisee wengine tuna kilo 80 mwezi wa 6 huu tunahaha kuzitoa ila zipo pale pale
 
Mkuu safuher kwanza nikushukuru sanaa kwa michango yako ya kuhimiza dondoo kadhaa za kupunguza mwili, sasa ni takribani mwezi na wiki tatu nimekuwa nikuata kanuni yako ya "kula unapojisikia njaa" na yafuatayo ndio matokeo niliyoyapata.

1. Ule ulafi wa hovyo kwa hovyo wote umepotea, zamani nakiri kusema nilikuwa food monger[emoji36], yani kula ilikuwa ugonjwa wangu mkubwa hasa nyama choma na vyakula vyenye mafuta, sasa ile appetite imepotea kabisa, mwili umeadapt intake ndogo ya chakula. kuna muda mpaka napitiliza mida ya kula naamua tu nile matunda + maji ili tumbo lisikae tupu.

2. Katika hali ambayo imenishangaza nimepoteza takribani kilo 9 pasipo mazoezi ya maana only kwa kufuatisha kanuni ya kuzuia ulaji wa hovyo kwa hovyo, wakati naanza programme hii nilikuwa na kilo 76 sasa nina kilo 67 huku malengo yangu ikiwa kufikisha 65. Hapa mpaka mwisho wa mwezi najua nitakuwa nishatimiza lengo [emoji1]

3. Mwili umekuwa mwepesi sanaa, sasa naonekana kijana zaidi, zile shikamoo zisizostahili nilishazichoka, nilikuwa naonekana "blooo" tofauti na umri wangu. , sasa nakuwa huru hata kuvaa tshirt na mashati mepesi tofauti na mwanzo, si kama nilikuwa na kitambi cha kutisha, la hasha! Lakini kwa umri wangu ningeendelea kidogo nilikuwa nafika pabaya then changamoto nyingine sisi wengine tumenyimwa kimo, urefu wangu ni 5.3'f ,1.6meter, ningekuwa na kimo zaidi ya hapo nisingeumiza kichwa na mwili.

Changamoto

Changamoto kubwa ninayoiona, ni je nitaweza kumaintain uzito huu, maana sisi wengine miili yetu, hata kwenye stress zone bado inatanuka tu, lakini pia adui mkubwa ambae ananikabiri ni Unywaji wa pombe, nyama kidogo nimepunguza lakini swala la kuacha beer limekuwa changamoto,

kawaida yangu atleast kila siku au baada ya siku moja lazima nipige atleast beer mbili ndio nikalale, baada ya kuanza utaratibu huu sasa beer naanzia friday-sunday lakini bado nichangamoto sanaa, beer imekuwa sehemu ya maisha yangu.

All in all naweza kusema hiki nilichokifanya kwa mwezi huu mmoja na nusu kimenibadilisha sana kwa upande wa kula yangu na kiufupi naenjoy sanaa coz point sio kuacha kula baadhi ya vyakula hapana, unakula kwa utaratibu na pale unaposikia hamu au ulazima wa kula na muda mwingine jilazimishe kula matunda ukiona njaa imezidi sana na taratibu unazoea, kuanzia Friday nimejiwekea ndio muda wa kuchafua tumbo, nyama choma, zege, biriani na makorokoro yote ndio muda wake then weekdays tunarudi kwenye utaratibu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera sana hiyo formula kuna mtu niliwahi kumpa hakuamini.

Kama muislamu kuna zile funga za kujitolea kama vile jumatatu na alhamisi hakikisha hazikupiti sinasaidia sana kukufanya uweze kujicontrol na kuona kuwa kula ni jambo la kawaida bila kuacha ramadhani.

Ukila unapojisikia njaa hata ule chipsi bado Kuna vitu mwili unahitaji kutoka katika chipsi,ni sawa na mwenye njaa atakula hata chakula asichopenda ndo hivyo hivyo mwili unapohitaji chakula hauchagui chipsi wala pilau wana ndizi.

Mtu anaekula kula ovyo ndo anatakiwa aangalie anachokula,ila mlaji wa utaratibu asiyrkula ovyoovyo aaah anaweza kula chochote kile.

Sasa ili ku maintain your appearance you have to take it as your behaviour.

Na ili iwe behaviour basi lazima ikite katika halmashauri ya mwili wako.
Kwa sasa hakuna njia ya kukufanya uzowee isipokuwa kujizoesha.

Na maana ya kujizoesha ni kujilazimisha jambo usilozoea wala kufeel comfortable unapifanya ili ufeel comfortable huko mbeleni.

Kwa sasa if you want to maintain your appearance and weight , you have to maintain your behaviour that gives you that weight.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa ulichozungumza kaka, kikubwa ni kufanya iwe behaviour na usichukulie kama ni mateso 😄 yani ifike kipindi uenjoy huo utaratibu, inshaalah na ramadhani hii nitafunga yote panapo majaaliwa na uzima.
Niweke mkazo kwa wale wavivu wa mazoezi utaratibu huu ni utaratibu bora kabisa, hata mazoezi ukifanya pasi kucontrol utaratibu wa kula ni kazi bure.
 

Nitafanya ivyo mkuu, wengine si wapigaji sana wa picha.

Naamini utapunguza tu hizo kilo, wewe utaratibu huu haukusumbui.😃
 
Mabadiliko yanaanza na wewe. Mimi nimeweza kubaki na kg 72 kwa muda zaidi ya miaka 15. Siri kubwa ni mazoezi na kutokula hovyo. Mimi sio mlaji naweza hata kusahau kula.

Nikiongezeka sana 74kg, nikipungua sana 70kg. Kikawaida nakuwa na 72kg
Middle weight.
 
Asante sana kwa ushuhuda, hizi ndio aina za mada zinazopaswa kujadiliwa mara kwa mara hapa JF, mada chanya na zenye kujenga, asante na hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…