Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Nina urefu wa sentimita 167 uzito wangu ni 70 kg najiona mzito sana . Je nifanyaje nipungue nashindwa sana sana kufanya mazoezi deily.
Ruka kamba na pia punguza unywaji usiku kama vile bia na soda ,kingine penda kufanya kazi za kutoa jasho...
 
Kwa mazoezi ya kutembea, kuruka kamba, jogging ilikuwa kila siku na zoezi lake pamoja na kupunguza wanga Nimefanikiwa kupunguza kg 11 kutoka disemba 17 2020 Hadi April 09,2021
 
Ngoja niwaambie kitu kuhusiana na Diet na kupunguza mwili...watu wengi wana amini ku acha kula mlo mmoja kunaweza kukakufanya upungue SIO KWELI
...Kama unaamua kufanya diet kwa ajili ya kupungua mwili fanya yafuatayo
...Punguza kula vyakula vyenye asili ya wanga na sukari...tumia kipimo cha ngumi yako(yaani kula ugali au wali size ya ngumi yako)...unatakiwa ule sana mboga za majani na samaki(nyama nyeupe)
...mboga za majani hazina madhara kula kwa wingi uwezavyo...kula sana matuda yatakusaidia kupata nyuzi nyuzi(fibers)...hizi husaidia kusaga chakula kwa haraka
Hujaelewa?...Fanya hivi
Asubuhi ukiamka jitahidi upate grass moja ya maji ya uvugu vugu(ukiitia ndimu au tangawizi ni bora zaid)
...Chai yako unaweza kula siles ya mkate moja au chapati moja au andazi 1(shughuli enhee[emoji23] ndo unapunguza wanga hivo)
...Mchana kula ugali size ya ngumi yako na mboga za kutosha pamoja na matunda...ukijisikia njaa kula tena ,ukijisikia tena njaa kula(kula size ndogo ya chakula utakapojisikia njaa...usile mpaka ukashiba sana
...Sema hapana kwa chips
....sema hapana kwa soda
.....Sema hapana kwa nyama nyekundu(ya ng'ombe,mbuzi
.....Kunywa maji mengi
.....kula kuku(bila ya ngozi yale)
FANYA MAZOEZI ...narudia tena FANYA MAZOEZI
...Kwa wale ambao wanasema wanafunga kupunguza uzito ni kweli kufunga kunapunguza mafuta mwilini....kivipi? Kipi unatakiwa ufanya check hpa[emoji1484]
...Kwa kawaida mwili wa binadamu huchukua masaa 8 kumaliza chakula kilichopo tumboni na kuanza kutumia mafuta yaliyo mwilini(kwenye cell)....hivo kama unataka utumie funga kumaliza mafuta mwilini hakikisha unafungulia na vyakula vyenye virutubisho na si wanga
Kivipi? Mfano umekula daku saa 8 usiku....uka kaa na njaa mpaka saa 12 jioni maana ake kuna mafuta yashatumika mwilini hivyo basi jitahidi hiyo saa kumi na mbili jioni ufungua kwa maji ya uvuguvugu(umeona enhee huwa tunafakamia ya baridi hapa[emoji23])...futari yako iwe nyepesi kama ni viazi viwe viwili mboga za majani na matunda kwa wingi
Kwa nini watu wanafeli?...watu wengi wanafunga lakini wanafungua kwa futari nzito na soda mpaka tumbo lina jaa...huwezi KUPUNGUA...kwa leo ni hayo(unaweza nirekebisha pia maana mimi sio mtaalamu wa rishe) nimeshea tu uzoefu maana nilikuwa mnene wazee[emoji23][emoji23]...nikitembea hatua mbili tu jasho naweza hata mwagilia mchicha
...Nikipata muda nitakuja niwaambie kuhusu Supu ya kabichi na kupunguza unene(japo mm ilinishinda[emoji23][emoji23][emoji23])...wewe sikukatishi tamaa....jambo la kuzingaitia USITUMIE MADAWA YA KUPUNGUZA UNENE....ntakuja hapa kuelezea madhara yake


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu iyo supu ya kabichi ndo ipoje nipe elimu tafadhari.
 
Kwa miezi hii minne iliyopita hadi kufikia Januari hii nimeweza kupunguza kilo 7, kutoka kilo 86 hadi 79.

Tupende mazoezi, tujiepushe na kula ovyo hasa vyakula vya mafuta na ikiwezekana ratiba za chakula muda wa jioni tusile milo mizito na matunda ndio yachukue nafasi ya milo ya jioni.

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
Kwasasa nina kilo 77, natakiwa bado niendelee kupunguza 5. [emoji2365][emoji2365][emoji2365]
 
Mimi nilipungua from 92kg to 68kg bila zoezi
Niliacha wanga na sukari kwa miezi 6
Nakula mihogo na mboga za majani for lunch,asubui mayai na maji ya moto au matunda tu usiku ni veggies na nyama za kuchemsha
Plus kunywa maji mengi ili upate choo,unavyozidi kupata choo unapungua kirahisi
 
Mimi nilipungua from 92kg to 68kg bila zoezi
Niliacha wanga na sukari kwa miezi 6
Nakula mihogo na mboga za majani for lunch,asubui mayai na maji ya moto au matunda tu usiku ni veggies na nyama za kuchemsha
Plus kunywa maji mengi ili upate choo,unavyozidi kupata choo unapungua kirahisi
Hongera
 
Wamama wajawazito. Kunyonyesha mtoto miezi 6 bila kumpa chochote kunasaidia kupunguza uzito ulikuja na ujauzito.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ni kweli mimi huwa napungua sana nikishajifungua japo kuwa miezi ya mwisho navimba sana sana lakini ukiniona baada ya miezi 3 huwezi amini kama ndo yule
 
mimi nilipungua kutoka 73-63 kwa mwezi mmoja tu, niliacha kula vyakula vyenye wanga kabisa
 
Mimi urefu wangu ni 165cm,uzito ni 54kg... i hope BMI yangu itakua normal.
 
mimi nilipungua kutoka 73-63 kwa mwezi mmoja tu, niliacha kula vyakula vyenye wanga kabisa
lakini kumbuka wanga inahitajika kwa kiasi chake mwilini angalia usije ukaanguka ghafla kwa kukosa sukari
 
Ukiweza kuachana na vyakula vya wanga na vyakula vyenye sukari basi utaweza kupunguza kilo pamoja na mwili ...naitakuwa rahisi hata kuchoma mafut ya mwili wakati wa kufanya mazoezi
 
Mabadiliko yanaanza na wewe. Mimi nimeweza kubaki na kg 72 kwa muda zaidi ya miaka 15. Siri kubwa ni mazoezi na kutokula hovyo. Mimi sio mlaji naweza hata kusahau kula.

Nikiongezeka sana 74kg, nikipungua sana 70kg. Kikawaida nakuwa na 72kg
Mwanzo ulikuwa na kilo ngapi??.
 
Nilikuwa na kilo 98 bonge la kitambi,Bonge la paja,bonge la mkono,...watu mtaani wakaanza kuniita bonge...hamna kitu kiliniuma kama kuitwa bonge...nkaanza mazoez nkashindwa mwlili mzito viungo vinauma...jaribu diet nikashindwa njaa inauma mpaka kizunguzungu nkakata tamaa....mda ukapita ...watu wanazid kuniita bonge...

Nikaenda gym nkaambiwe nilipie elfu 80 kwa mwezi...nkaenda benk kuchukua pesa...huwez hamini niliiangalia ile pesa mkononi nkasema yaani naenda kutoa elfu 80 gym wakati viwanja viko bure tuu!?[emoji848]...nkazama mtumbani nkanunu raba rut ikaanza...Kimbia sana mwez mzima nkapungua kilo 3...nkasema ahaaa kumbe inawezekana nkapata na elimu ya lishe....ratiba ikawa hivi

....Nikapunguza vyakula vya wanga yaani ugari nilikuwa nakula saizi ya ngumi yangu...mboga za majani kwa wingi sna yaana
.....Nilikuwa nakula pale nnapojisikia njaaa(watu weng tumezoea kula mara tatu kwa siku lakini chakula tunachokula ni kingi so kinakutana tumbon) Ki afya unaruhusiwa kula hata mara sita kwa siku lakini kidogo kidogo(unapojisikia njaa$

.....Nikaacha kabisa soda na nyama nyekundu(baadae sana nkaanza kutumia maana ukiwa kwenye mazoez ya kupunguza mwil kuna kitu kinaitwa 'cheating day'

......Ratiba yangu ya mazoez ilikuwa kila sku asubuhi saa kumi na moja nkiamka kufanya ibada naamkia kiwanjani ...kukimbia,kuruka kamba,na mazoez ya viungo(Asikuambie mtu zoez la kukimbia ndo zoez bora la kupunguza uzito
....Jioni nkirud kazini naingia tena kiwanjani

....Nkawa fiti kuna kipind nkawa na uwezo wa kukimbia mpaka round 30 za kiwanja....nkisem nkimbie road work nnawez kimbia mpaka km 20,15
...Nikapungua kilo pamoja na uzito nkawa na mwili mdogo na wa kawaida....nikawa na enjoy maisha

...Kutokana na hari ya kuwa na pumzi ya kutosha nakanza kucheza football
Sasa mpira wetu wa uswahilini upati mda wa kujiandaa unatoka nyumbani kiwanjani....sipati mda mwing wa kufanya mazoez sana(nacheza beki ya kati)...ka mwili kamerud kidooogo sema ka kawaida sio mnene[emoji2]
...MUHIMU...ukiitaka kupunguza uzito

...Punguza ulaji wa sukar na wanga
....kula sana mboga za majani kunywa sna maji
.....fanya mazoez
Ukipungua kwa kufanya mazoez na kufuata lishe unakuwa phyisical...ukifanya tu diet unapingua kama mgonjwa mgonjwa hivi...haui physical yaani[emoji23]...so fanya yote

Ukishachanganya mazoez chagua siku ambayo utaaita 'cheatind day' hii siku usifanye diet wala usifanye mazoez yaan kula tu junk...masoda kula chips kula,nyama hata kilo we kula(japo unywe maji meng).....huo ndo ushuhuda wangu wakuu...na kipind unajizuia kula vitu vya sukari utakuta mwili unatamani kula vitu vya sukari...tumia Tende zitakupunguzia tamaa ya kula sukari
....vitu vingine namna ya kunywa maji...kunywa maji nusu saa kabla ya kula na nusu saa baada ya kula....nini faida yake?....

kunya maji kabla ya kula kutakufanya upunguze hamu ya kula...hivo hutokula chakula kingi....kinywa baada ya kula kutakusaidia digestion ifanyike kwa urahisi...tumezoea kunywa maji tukimaliza tu kula hii nimbaya maana inaifanya utumbo kuwa mtepemtepe hivo kupunguz digestion
....kula matunda kwanz alafu chakula na sio chakula alafu matunda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera Sana Mkuu, ngoja nami nijaribu.
 
Back
Top Bottom