Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Nina urefu wa sentimita 167 uzito wangu ni 70 kg najiona mzito sana . Je nifanyaje nipungue nashindwa sana sana kufanya mazoezi deily.
Ruka kamba na pia punguza unywaji usiku kama vile bia na soda ,kingine penda kufanya kazi za kutoa jasho...
 
Kwa mazoezi ya kutembea, kuruka kamba, jogging ilikuwa kila siku na zoezi lake pamoja na kupunguza wanga Nimefanikiwa kupunguza kg 11 kutoka disemba 17 2020 Hadi April 09,2021
 
Mkuu iyo supu ya kabichi ndo ipoje nipe elimu tafadhari.
 
Kwasasa nina kilo 77, natakiwa bado niendelee kupunguza 5. [emoji2365][emoji2365][emoji2365]
 
Mimi nilipungua from 92kg to 68kg bila zoezi
Niliacha wanga na sukari kwa miezi 6
Nakula mihogo na mboga za majani for lunch,asubui mayai na maji ya moto au matunda tu usiku ni veggies na nyama za kuchemsha
Plus kunywa maji mengi ili upate choo,unavyozidi kupata choo unapungua kirahisi
 
Hongera
 
Wamama wajawazito. Kunyonyesha mtoto miezi 6 bila kumpa chochote kunasaidia kupunguza uzito ulikuja na ujauzito.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ni kweli mimi huwa napungua sana nikishajifungua japo kuwa miezi ya mwisho navimba sana sana lakini ukiniona baada ya miezi 3 huwezi amini kama ndo yule
 
mimi nilipungua kutoka 73-63 kwa mwezi mmoja tu, niliacha kula vyakula vyenye wanga kabisa
 
Mimi urefu wangu ni 165cm,uzito ni 54kg... i hope BMI yangu itakua normal.
 
mimi nilipungua kutoka 73-63 kwa mwezi mmoja tu, niliacha kula vyakula vyenye wanga kabisa
lakini kumbuka wanga inahitajika kwa kiasi chake mwilini angalia usije ukaanguka ghafla kwa kukosa sukari
 
Ukiweza kuachana na vyakula vya wanga na vyakula vyenye sukari basi utaweza kupunguza kilo pamoja na mwili ...naitakuwa rahisi hata kuchoma mafut ya mwili wakati wa kufanya mazoezi
 
Mabadiliko yanaanza na wewe. Mimi nimeweza kubaki na kg 72 kwa muda zaidi ya miaka 15. Siri kubwa ni mazoezi na kutokula hovyo. Mimi sio mlaji naweza hata kusahau kula.

Nikiongezeka sana 74kg, nikipungua sana 70kg. Kikawaida nakuwa na 72kg
Mwanzo ulikuwa na kilo ngapi??.
 
Hongera Sana Mkuu, ngoja nami nijaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…