Shuhudia 'vibe' la wananchi na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiwa katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Katika uzinduzi wa kampeni hizo, mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CUF, Gombo Samandito Gombo na Mgombea Mwenza wake Husna Abdalla wataanza rasmi kuzinadi sera zao.