Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mshambuaji wa Polisi Tanzania FC, Ditram Adrian Nchimbi (Duma), amegeuka gumzo nchini baada ya jana Oktoba 3, 2019 kuwanyosha vilivyo Yanga SC mabao matatu peke yake Hat-Trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-Trick msimu huu wa VPL, 2019/2020.
Taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania TFF, ni kwamba, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Ettiene Ndairagije amemuongeza kikosini Ditram Adrian Nchimbi, tayari kwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA, Oktoba 14, 2019 dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda, utakaochezwa Jijini Kigali.