Shujaa wa Hat-Trick dhidi ya Yanga SC, Ditram Nchimbi aongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars

Shujaa wa Hat-Trick dhidi ya Yanga SC, Ditram Nchimbi aongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mshambuaji wa Polisi Tanzania FC, Ditram Adrian Nchimbi (Duma), amegeuka gumzo nchini baada ya jana Oktoba 3, 2019 kuwanyosha vilivyo Yanga SC mabao matatu peke yake Hat-Trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-Trick msimu huu wa VPL, 2019/2020.

Taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania TFF, ni kwamba, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Ettiene Ndairagije amemuongeza kikosini Ditram Adrian Nchimbi, tayari kwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA, Oktoba 14, 2019 dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda, utakaochezwa Jijini Kigali.
IMG_20191004_114910_791.jpeg
IMG_20191004_114846_117.jpeg
 
Uwezo wake na umahiri wake uwanjani ndo umemuinua huyo Nchimbi.![emoji23][emoji23][emoji23]
Mmmh!! Mtani hivyo unadhani ilikuwepo haja ya kuzungumzia aliyoyafanya jana ikiwa kainuliwa na umahiri wake?
 
Ndala ndo wenye shida ya Streka, haifungi mpaka mipira ya kutengwa au golikipa atoe boko..[emoji23]
Sasa duniani kwote, fundi wa kabumbu ya sayansi ni yule anayepiga mipira ya kutenga. Achana na hizi mshike mshike mkamate full vurumai a.k.a sandakalawe.

Kumbe faulo ikipigwa tumbo huwa linakuwaka moto eeeh?
 
Mshambuaji wa Polisi Tanzania FC, Ditram Adrian Nchimbi (Duma), amegeuka gumzo nchini baada ya jana Oktoba 3, 2019 kuwanyosha vilivyo Yanga SC mabao matatu peke yake Hat-Trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-Trick msimu huu wa VPL, 2019/2020.

Taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania TFF, ni kwamba, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Ettiene Ndairagije amemuongeza kikosini Ditram Adrian Nchimbi, tayari kwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA, Oktoba 14, 2019 dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda, utakaochezwa Jijini Kigali.View attachment 1223327View attachment 1223328
Upumbavu wa kiwango cha lami
 
Mimi naona ni sawa tu. Tuwe tunajaribu washambuliaji wanaojitokeza kila mara hatimaye atapatikana mmojawapo atakayekuwa na jicho la goli. Ukiaangalia washambuliaji karibu wote wazuri kwenye ligi ya bongo wameshaitwa timu ya taifa lakini wanachokosa ni utulivu mbele ya goli. Huenda Ditram akawa ndiye mshambuliaji tunayemtafuta sana kwa sasa.
 
Anastahili kuanza hata kwenye hiyo mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda. Ni mchezaji mpambanaji sana awapo uwanjani. Bahati mbaya hakuwa na bahati ya kuonekana mapema. Labda ni kwa sababu ya kuchezea timu za chini kwa muda mrefu.
 
Naona kuwa hata yeye Nchimbi ashaona kuwa hii ndo fursa sasa ya kuonyesha makali yake..Yale mabao yake yalikuwa safi yasiyo shaka hata kidogo..!

Tukiwaamini na wao Watajiamini
 
Back
Top Bottom