Mchukueni mikia ili afunge tena kila mechi kama jana.
Jionee chenga ya mateso bila chuki..embu nipe mrejesho lilikuwa bao la ngapi hapo..!View attachment 1223415
Mmmh!! Mtani hivyo unadhani ilikuwepo haja ya kuzungumzia aliyoyafanya jana ikiwa kainuliwa na umahiri wake?Uwezo wake na umahiri wake uwanjani ndo umemuinua huyo Nchimbi.![emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa duniani kwote, fundi wa kabumbu ya sayansi ni yule anayepiga mipira ya kutenga. Achana na hizi mshike mshike mkamate full vurumai a.k.a sandakalawe.Ndala ndo wenye shida ya Streka, haifungi mpaka mipira ya kutengwa au golikipa atoe boko..[emoji23]
Upumbavu wa kiwango cha lamiMshambuaji wa Polisi Tanzania FC, Ditram Adrian Nchimbi (Duma), amegeuka gumzo nchini baada ya jana Oktoba 3, 2019 kuwanyosha vilivyo Yanga SC mabao matatu peke yake Hat-Trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-Trick msimu huu wa VPL, 2019/2020.
Taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania TFF, ni kwamba, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Ettiene Ndairagije amemuongeza kikosini Ditram Adrian Nchimbi, tayari kwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA, Oktoba 14, 2019 dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda, utakaochezwa Jijini Kigali.View attachment 1223327View attachment 1223328
alisikika shabiki mmoja wa yanga akilalamika kwa uchungu........Upumbavu wa kiwango cha lami
Naona kuwa hata yeye Nchimbi ashaona kuwa hii ndo fursa sasa ya kuonyesha makali yake..Yale mabao yake yalikuwa safi yasiyo shaka hata kidogo..!Anastahili kuanza hata kwenye hiyo mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda. Ni mchezaji mpambanaji sana awapo uwanjani. Bahati mbaya hakuwa na bahati ya kuonekana mapema. Labda ni kwa sababu ya kuchezea timu za chini kwa muda mrefu.