Shujaa wa Hat-Trick dhidi ya Yanga SC, Ditram Nchimbi aongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars

Hawezi kuwa na maoni, aliko huko ametepeta vilivyo..!
Maoni ya kukosoa utaratibu wa kusubiria wachezaji shamba la bibi ama Kwa mchina yako palepale.Nchimbi kacheza more than two premier league seasons and for more than two premier league teams kama kuna scouting kwanini hakuonekana hadi alipocheza Dar? Ni wangapi wako kama Nchimbi na hawajaonekana?Big mind discuss issues not individuals and not incidences.
 
Current Best striker in Tanzania


1. Nchimbi
2. Ayee
3. Kelvin John
4. Simchimba
5. Msuva Simon
6. Samatta
7. Onesmo mayaya
 
Unaona mbali mkuu
Ni kweli mkuu. Kutumbukiza mpira golini huwa mtu hafundishwi ni kipaji mtu anazaliwa nacho. Unaweza fika mara kumi golini ndani ya hatua sita usifunge goli hata moja mwenzio akafika nje ya kumi nane mara moja tu akafunga goli. Kwa wale waliocheza mpira hata madaraja ya chini au shuleni wanajua hili jambo, pale golini sijui huwa kunawekwa nini kinachopteza utulivu kwa washambuliaji yaani unaweza kukokota mpira ukawapiga chenga mabeki wote ukabaki na kipa halafu ukapiga nje. Ukifuatilia ligi kuu bara utaona kuna mafowadi wawili tena wa kimataifa sipendi kuwataja wao wanacheza vizuri sana lakini inapofika kutumbukiza tu mpira golini sehemu ambayo mtoto wa miaka mitatu anaweza kuugusa ukaingia lakini wao kwao inakuwa utata kiasi ambacho unaweza sema labda wamelogwa. Lakini hapana wao si wamaliziaji bali wao ni washambuliaji machachari ambao wanahitaji awepo mmaliziaji kati yao wao wampe tu assist.

Ninachokiona kwa Ditram huenda ni mmaliziaji tuliyemkosa Tanzania baada ya muda mrefu ukiacha Samata nafikiri tumpe muda tuuone mwendelezo wake japo kashatuonyesha kuwa anaweza.

Washambuliaji wamaliziaji siku hizi wamekuwa adimu sana kuwataja wachache waliowahi kucheza ligi ya bongo ni Mogela, Ambani, Emmanuel Gabriel, Mohamed Hussein, Amisi Tambwe na wengineo, na kwa sasa yupo Kagere. Kwa kawaida wamaliziaji wao hawana vitu vingi sana na unaweza usiwaone uwanjani kwa dakika zote 89 za mchezo ila kabla refa hajamaliza kupuliza kipenga cha mwisho utashangaa ubao unasoma goli.
 
Na kuna mshambuliaji mwengine ametajwa hapo juu na mdau mmoja anaitwa Paul Nonga a.k.a baba Paroko nadhani naye ni wakati muafaka kwa makocha wakamfuatilia na kumjaribu kwenye mechi za kirafiki za kimataifa ili wamuone huenda akawafaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…