Shujaa wa kike aliyefukuza Wajerumani kwa kutumia nyuki

Shujaa wa kike aliyefukuza Wajerumani kwa kutumia nyuki

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Serikali ya Mkoa wa Singida imefanya uamuzi wa kubadili jina la uwanja wa mpira wa MAMFUA STADIUM na sasa umepewa jina la LITTI STADIUM ikiwa ni hatua muhimu za kumuenzi mwanamke shujaa wa Singida aliyepigana na wakoloni wa Kijerumani kwa kutumia nyuki kama silaha ya mapambano.

LITTI alikuwa ni mwanamke shujaa aliyepigana na Wajerumani kwa kulinda himaya ya Wanyaturu akipinga utaratibu wa kupora ng'ombe, kupora nafaka, kutumikisha watu na kutoza kodi uliofanywa na wakoloni wa Kijerumani miaka ya 1907 - 1910.

Mwanamke huyu alifanikiwa kuwashinda Wajerumani kwenye mapambano mawili kwa kuwafurumushia nyuki na kuwaua baadhi ya askari ya Kijerumani. Pambano la tatu LITTI alisalitiwa na mtu wake wa karibu aliyetoa siri kwa Wajerumani na kufanikiwa kumkamata na kumchinja.

Kichwa cha mwanamke huyu kilichukuliwa kupelekwa Ujerumani hadi leo hakijarejeshwa Tanzania.

Tunaendelea kuwaibua mashujaa wetu ili waweze kutambuliwa na kuenziwa kwenye historia ya mkoa wa Singida na nchi yetu.
 
Ni kweli kabisa kaka. Ni ukweli mtupu ulichoeleza cha kuongezea ni kwamba adi leo pale ilipokua nyumba yake hakuna kitu chochote au jengo lililojengwa kwa sababu kila pakijengwa jengò huwa lina dondoka.
 
Ni wapi hapo Singida?
 
Mtoa mada, hujasema ni Siri gani huyo msaliti alitoa
 
Back
Top Bottom