Shujaa wa kike aliyefukuza Wajerumani kwa kutumia nyuki

Shujaa wa kike aliyefukuza Wajerumani kwa kutumia nyuki

Leo hii mashujaa wetu Zitto na Lissu wako busy nawo?
Inaskitisha sana sana.
 
Ni kweli kabisa kaka. Ni ukweli mtupu ulichoeleza cha kuongezea ni kwamba adi leo pale ilipokua nyumba yake hakuna kitu chochote au jengo lililojengwa kwa sababu kila pakijengwa jengò huwa lina dondoka.

No nyumbaa mwili wake ulipozikwaa pasina kichwaa haijawahi kuangukaa Bali wakiwekaa mababati au ezekoo huwa linanyofokaa kill mwakaa Hadi saivi wamechokaa kuwekaa wamaliachaa wazii
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Sasa brooo huku ni kututukanaa wanyaturuu angalia kauli zakoo
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Mkuu kwani uchawi ni tusi?kila jamii wachawi wapo .....any way mnisamehe wanyaturu shemeji zangu
 
Serikali ya Mkoa wa Singida imefanya uamuzi wa kubadili jina la uwanja wa mpira wa MAMFUA STADIUM na sasa umepewa jina la LITTI STADIUM ikiwa ni hatua muhimu za kumuenzi mwanamke shujaa wa Singida aliyepigana na wakoloni wa Kijerumani kwa kutumia nyuki kama silaha ya mapambano.

LITTI alikuwa ni mwanamke shujaa aliyepigana na Wajerumani kwa kulinda himaya ya Wanyaturu akipinga utaratibu wa kupora ng'ombe, kupora nafaka, kutumikisha watu na kutoza kodi uliofanywa na wakoloni wa Kijerumani miaka ya 1907 - 1910.

Mwanamke huyu alifanikiwa kuwashinda Wajerumani kwenye mapambano mawili kwa kuwafurumushia nyuki na kuwaua baadhi ya askari ya Kijerumani. Pambano la tatu LITTI alisalitiwa na mtu wake wa karibu aliyetoa siri kwa Wajerumani na kufanikiwa kumkamata na kumchinja.

Kichwa cha mwanamke huyu kilichukuliwa kupelekwa Ujerumani hadi leo hakijarejeshwa Tanzania.

Tunaendelea kuwaibua mashujaa wetu ili waweze kutambuliwa na kuenziwa kwenye historia ya mkoa wa Singida na nchi yetu.
Tabia ya wanyaturu ya kusaliti hata kama wote muko pamoja kumbe ni ya damuni, huyo mnyaturu mwenzake aliyemsaliti alifanya vibaya sana sasa hivi historia inamuhukumu na kizazi chake.Najaribu kufanya connection ya dot. na hali ya sasa hivi wasaliti bado wapo kwenye hiyo kabila ya wanyaturu.
 
Majina mengi ya Kinyaturu yanashindikana kuandikika kwa Kiswahili na hiyo kupoteza kabisa uhalisia wa jina.
Huyu shujaa wa kike jina lake linaandikwa Litti, lakini kwa matamshi ya Kinyaturu halitamukwi hivyo.
Kwa Kinyaturu unaweza kuliandika , LEETRI na siyo Litti.
Waliompa heshima hii wafanye marekebisho tafadhali.
 
Wale ambao walikuepo wakati tunapigana vita ya Uganda, wajue kabisa tulitumia mbinu mbali mbali pamoja na kamati za ufundi kumshinda Iddi Amini. Wakati wanafanya upelelezi, askari wetu waliweza kuwafikia askari wa Iddi Amani bila kuonekana na baadaye kupata mbinu ya kuwashambulia kwa urahisi.
Unapotetea maslahi ya wengi kwa kutumia nguvu za Kimungu au kamati za ufundi hatuiti ni uchawi ila tunasema ni utaalamu wa asili au nguvu za Mungu.
Musa, katika Agano la kale kwenye Biblia Takatifu, imeandikwa kuwa alipiga bahari kwa fimbo yake na ikagawanyika na Wana wa Isreael wakapita. Wamisri walipokuja nyuma yao Abrahamu alipiga tena maji na yakawafunika Wamisri. Huu haukuwa uchawi bali nguvu za Kimungu.
 
Serikali ya Mkoa wa Singida imefanya uamuzi wa kubadili jina la uwanja wa mpira wa MAMFUA STADIUM na sasa umepewa jina la LITTI STADIUM ikiwa ni hatua muhimu za kumuenzi mwanamke shujaa wa Singida aliyepigana na wakoloni wa Kijerumani kwa kutumia nyuki kama silaha ya mapambano.

LITTI alikuwa ni mwanamke shujaa aliyepigana na Wajerumani kwa kulinda himaya ya Wanyaturu akipinga utaratibu wa kupora ng'ombe, kupora nafaka, kutumikisha watu na kutoza kodi uliofanywa na wakoloni wa Kijerumani miaka ya 1907 - 1910.

Mwanamke huyu alifanikiwa kuwashinda Wajerumani kwenye mapambano mawili kwa kuwafurumushia nyuki na kuwaua baadhi ya askari ya Kijerumani. Pambano la tatu LITTI alisalitiwa na mtu wake wa karibu aliyetoa siri kwa Wajerumani na kufanikiwa kumkamata na kumchinja.

Kichwa cha mwanamke huyu kilichukuliwa kupelekwa Ujerumani hadi leo hakijarejeshwa Tanzania.

Tunaendelea kuwaibua mashujaa wetu ili waweze kutambuliwa na kuenziwa kwenye historia ya mkoa wa Singida na nchi yetu.

Kwani hiyo NAMFUA STADIUM aina mana yeyote.
si wangetafuta kitu kingine wakipe jina hilo la LITTI.
 
Hongera sana Bibi Litti, endelea kupumzika kwa amani,

Historia ya Tanganyika imefichwa fichwa sana sijui kwanini.
 
Back
Top Bottom