figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Mmiliki wa mabasi ya ‘Zacharia’, Peter Zacharia, Juni 30, 2018 alishikiliwa na vyombo vya dola mkoani Mara kwa tuhuma za kuwamimini risasi maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa waliodai walikuwa katika majukumu yao. Matiss hao walikimbizwa hospitali ya mjini Tarime kupata matibabu
Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi
Awali ilidaiwa mfanyabiashara huyo alitekwa na watu wasiojulikana alipokuwa ofisini kwake katika moja ya vituo vyake vya mafuta mjini Tarime.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima aliwaambia Wanahabari kwamba, kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa usalama walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao
“Wenzao wawili walishuka kwenye gari ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo,” alisema Malima.
"Baada ya wenzao kujeruhiwa kwa risasi, maofisa wengine walifanikiwa kumdhibiti Zakaria na kumtia mbaroni na kumkabidhi kwa polisi.
Usalama wa taifa walienda kukagua mafuta kwani wao walikuwa Polisi?
Ilikuwa imepita siku chache baada ya Mwili wa Tajiri mwenzie wa huko huko Mara kuokotwa kwenye Kiroba
Kwa Wasiojua: March 14, 2018
mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Super Sami, Samson Josia alitoweka baadaye mwili wake ukapatikana katika Mto Ndabaka ukiwa umefungwa kwenye kiroba. Ilikuwa ni siku tano baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser kukutwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Zaidi Soma: Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba
Hivyo watu walikuwa bado wanahofu. Walipotaka kumteka, akawawahi na kuwamiminia Risasi. Watu wakajaa, ndo Polisi na Wananchi kujaa kama mnavyojua wenzetu wa Mkoa wa Mara. Watu wakajaa na Mapanga sime mawe na kila kitu. Polisi walipokuja ndo akajisalimisha na kupelekwa kituoni na Wale TISS wakapelekwa Hospitali. Tangia hapo Utekaji Mkoa wa Mara Ukakoma.
Ingekuaje Zakaria asingejitetea?
Kesi yake ilienda mwishoe akabambikizwa kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi. Peter Zakaria apata tabu sana. Sasa apata kesi ya uhujumu uchumi na kumiliki silaha nje ya sheria. Anyimwa dhamana...
Tangu Hayati Pombe Magufuli afe, kidogo Zakaria akaanza kupumua.
Ndo nikaanza kuelewa kwanini Rais Samia alikataa Urais wake usiwe awamu ya tano bali ya Sita.
Awamu ya tano ilinuka Mifereji ya damu iliyoganda.