Habari zenu wapendwa?
Napenda kuwashukuru wana JF wote kwa ushirikiano wenu na upendo wenu wa dhati kwangu. Mwaka Jana mwezi wa 12 nilileta uzi wangu nikiomba ushauri juu ya HIV.
Ilikuwa ni baada ya kukatwa na wembe bahati mbaya aliotumia mgonjwa na kwa kweli nilikuwa katika kipndi kigumu sana nilikuwa na msongo mkubwa wa mawazo. Nilikuwa nikishindwa hata kula na wengi mlinishauri nikapime ila nilikuwa naogopa nakubaki tu kulia, ila wana Jf mlikuwa mkinitia moyo sana katika wakati mgumu niliokuwa nikipitia.
Siku ya leo baada ya kuteseka sana na mawazo nilimuomba Mungu anipe ujasiri nikaenda kupima. Toka tukio linipate mwez wa 12 mpaka leo ni miez 5 nimepima nikakutwa negative.
Namshukuru sana Mungu kwa upendo wake kwa kunivusha salama katika hili nimeamini Mungu wetu halali wala kusinzia hakika Mungu ni mwema kwa wote.
Nawapenda sana ndugu zangu wana Jf Mungu atuzidishie upendo.