Shukrani: Baada ya kujikata na wembe wa muathirika wa VVU nimepima na kukutwa 'negative'

Shukrani: Baada ya kujikata na wembe wa muathirika wa VVU nimepima na kukutwa 'negative'

tembocard

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
247
Reaction score
121
Habari zenu wapendwa?

Napenda kuwashukuru wana JF wote kwa ushirikiano wenu na upendo wenu wa dhati kwangu. Mwaka Jana mwezi wa 12 nilileta uzi wangu nikiomba ushauri juu ya HIV.

Ilikuwa ni baada ya kukatwa na wembe bahati mbaya aliotumia mgonjwa na kwa kweli nilikuwa katika kipndi kigumu sana nilikuwa na msongo mkubwa wa mawazo. Nilikuwa nikishindwa hata kula na wengi mlinishauri nikapime ila nilikuwa naogopa nakubaki tu kulia, ila wana Jf mlikuwa mkinitia moyo sana katika wakati mgumu niliokuwa nikipitia.

Siku ya leo baada ya kuteseka sana na mawazo nilimuomba Mungu anipe ujasiri nikaenda kupima. Toka tukio linipate mwez wa 12 mpaka leo ni miez 5 nimepima nikakutwa negative.

Namshukuru sana Mungu kwa upendo wake kwa kunivusha salama katika hili nimeamini Mungu wetu halali wala kusinzia hakika Mungu ni mwema kwa wote.

Nawapenda sana ndugu zangu wana Jf Mungu atuzidishie upendo.

IMG_20180514_191652_800.JPG
 
hizo nyembe na vifaa vingine vinachangia kwa kiasi kidogo sana! yawezekana alitumia lakini wembe huo ulikaa masaa kabla haujatumia hivyo virusi haviwezi kuishi muda huo wote
Ulikaa dk 2 ndomana nilikuwa nachanganyikiwa ila Leo nilivyongea na doctor kaniambia virus vinakaa nje ya damu kwa sekunde 5 tu
 
Habari zenu wapendwa? Napenda kuwashukuru wana Jf wote kwa ushirikiano wenu na upendo wenu wa dhati kwangu, mwaka Jana mwezi wa 12 nilileta Uzi wangu nikiomba ushauri juu ya HIV ilikuwa ni baada ya kukatwa na wembe bahati mbaya aliotumia mgonjwa kwa kweli nilikuwa ktk kipndi kigumu sana nilikuwa na msongo Mkubwa wa mawazo nilikuwa nikishindwa hata kula na wengi mlinishauri nikapime ila nilikuwa naogopa nakubaki tu kulia ila wana Jf mlikuwa mkinitia moyo sana ktk wakati mgumu niliokuwa nikipitia, siku ya Leo baada ya kuteseka sana na mawazo nilimuomba Mungu anipe ujasiri nikaenda kupima toka tukio linipate mwez wa 12 mpaka Leo ni miez 5 nimepima nikakuta negative. Namshukuru sana Mungu kwa upendo wake kwa kunivusha salama ktk hili nimeamini Mungu wetu halali wala kusinzia hakika Mungu ni mwema kwa wote. Nawapenda sana ndugu zangu wana Jf Mungu atuzidishie upendo.View attachment 777296
sasa mungu na kupima kwako vina husisana nini, na je ungepata unge mshukuru tena au? USITAJE JINA LA BWANA MUNGU WAKO BURE
 
mm labda uyo mwathirika iyo wembe haikumjerui pindi ana itumia ndio maana uko salama
 
Back
Top Bottom