Shukrani kwa Jamii Forums kwa kunipa Tuzo 🙏🏽

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
966
Reaction score
6,019
Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.
IMG-20240922-WA0063.jpg
Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.
IMG-20240922-WA0122.jpg
Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.
IMG-20240922-WA0075.jpg
Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.
IMG-20240922-WA0123.jpg
Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
 
Attachments

  • IMG-20240922-WA0124.jpg
    IMG-20240922-WA0124.jpg
    176.9 KB · Views: 6
  • IMG-20240922-WA0091.jpg
    IMG-20240922-WA0091.jpg
    99.3 KB · Views: 6
  • IMG-20240922-WA0065.jpg
    IMG-20240922-WA0065.jpg
    101.5 KB · Views: 7
Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.

Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.

Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.

Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.

Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
GOD BLESS YOU TOO....
 
Hongera sana Dkt. Gwajima ( minister) mwenyezi Mungu akuongoze katika utendaji wako umekuwa Bora katika kusikiliza maoni na kufanyia kazi uzidi kuongezeka.
Ukipata nafasi washauri na fellow ministers kutumia mitandao ya kijamii kupata matukio, maoni na mitazamo tofauti na kufanyia kazi ili waongezeke kama wewe. Asante
 
Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.

Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.

Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.

Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.

Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
Safi hiyo tuzo ni kielelezo tosha kuwa mheshimiwa ni msikivu na unakubali kupokea changamoto na kuzifanyia kazi mara moja haijalishi ni muda gani na ni mfuatiliaji mzuri wa changamoto za waajiri wako wananchi wa tanzania!
 
Back
Top Bottom